logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ni sisi Wakisii tulifanya kesi ya Ezekiel iwe nyororo - Embarambamba

Nilimwambia sisi Wakisii ndio tulikusupport kwa court

image
na TOM KIRIMI

Habari26 June 2023 - 14:15

Muhtasari


  • •Kulingana na msanii huyo, alidakia kuwa wao ni majirani kutoka Kisii, huku akidai kwamba walichangia pakubwa katika kesi yake na hivyo kutolewa kwake mahakamani.

Mwimbaji wa nyimbo za injili Embarambamba, ameeleza kuwa jamii ya Wakisii ndiyo ilifanya kesi ya mhubiri aliyekumbwa na utata Ezekiel Odero wa kanisa la New Life Center iwe nyororo.

Embarambamba amekiri hilo kuputia mahojiano ya simu na Radio Jambo, alipokuwa akieleza sababu zilizochangia kufungwa kwa kwa akaunti yake ya YouTube.

Nilimwambia sisi Wakisii ndio tulikusupport kwa court, sisi ndio tulifanya kesi yake ikakuwa nyororo.” Alieleza.

Mhubiri huyo alikuwa amekamatwa miezi miwili iliyopita, kwa madai ya kueneza mahubiri ya itikadi kali kwa umma. Kulingana na taarifa zilizoibuka kutoka Mavueni Kilifi, Ezekiel alikuwa amekamatwa baada ya kuhojiwa kwa muda mrefu kwa madai kanisa lake linahusiana na uchawi.

Kulingana na msanii huyo, alidakia kuwa wao ni majirani kutoka Kisii, huku akidai kwamba walichangia pakubwa katika kesi yake na hivyo kutolewa kwake mahakamani.

Mhubiri huyo amekuwa katika hali ya sintofahamu kwa miezi miwili, tangu mahakama ilipoamuru kuzuiliwa kwake na kuendeleza uchunguzi kuhusu kanisa lake.

Ezekiel alipata afueni wiki chache zilizopita, baada ya kufunguliwa akaunti zake za benki pamoja na kufunguliwa kituo chake cha runinga.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved