logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Machozi, wafuasi wa Raila wakielekea Central Park

Msafara wa wafuasi Raila Odinga kuelekea Central Park wakakabiliwa na safari iliyojawa na machozi.

image
na TOM KIRIMI

Habari07 July 2023 - 12:15

Muhtasari


  • • Wafuasi hao wamekuwa wakitupiwa vitoza machozi kutoka kwa polisi ambao wanaonekana kuhakikisha wanafunga barabara zote zinazoelekea katikati mwa jiji la Naiobi.
Polisi wawatupia vitoza machozi kwa wafuasi wa Azimio katika barabara ya Jogoo Julai 7,2023.

Msafara wa wafuasi wa kiongozi wa Azimio Raila Odinga kuelekea Central Park wakakabiliwa na safari iliyojawa na machozi polisi wakijaribu kuwazuia kufika katikati ya mji.

Wafuasi hao wamekuwa wakitupiwa vitoza machozi kutoka kwa polisi ambao wanaonekana kuhakikisha wanafunga barabara zote zinazoelekea katikati mwa jiji la Naiobi.

Picha za moja kwa moja hadi saa 2:10 jioni zinaonyesha waandamanaji wakijaribu kufunika nyuso zao ili kupunguza athari za vitoza machozi kutoka kwa polisi.

Waandamanaji hao wanatembea kutoka eneo la Kamukunji kuelekea Gikomba ambapo wanatarajia kufikia barabara zinazoelekea CBD.

Wengine wanaonekana wakifunika mapua na sweta zao ili kuzuia gesi hiyo kuwaathiri. Licha ya shambulizi hilo wafuasi hao walonekana kutobabaishwa baada ya kupata maji ili kupunguza athari za gesi hiyo kali na kuendelea na safari yao.

Wakati fulani, mtu anasikika akiwataka maafisa wa polisi kufuata sheria.

"Mfuate sheria na msitumiwe vibaya tafadhali," anasema.

Katika viwanja vya Kamukunji, Raila aliwaamuru wafuasi wake kutumia njia yoyote inayowezekana kufika Central Park.

"Kuna njia nyingi za kufikia 'Rome', wakati wanazuia barabara moja, tunatumia nyingine. Leo, 'Rome' yetu inaitwa Central Park, hapo ndipo tutakutana baada ya mkutano wa Kamukunji," alisema.

Kiongozi huyo wa upinzani pia amewataka waandamanaji kukumbatia amani katika safari yao.

Takriban saa 2:36 jioni, msafara ulikuwa katika eneo la Ngara.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved