logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Fahamu tunda lenye uwezo wa kuimarisha tendo la ndoa

Zabibu ina uwezo wa kuongeza nguvu za kiume hivo kuboresha tendo la ndoa.

image
na Davis Ojiambo

Habari13 July 2023 - 05:51

Muhtasari


  • • Zabibu nyeusi, huboresha mtiririko wa damu,' anasema hivyo kutibu tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
  • • Utafiti mwingine pia ulionyesha kuwa zabibu nyeusi inaweza kusaidia kuondoa harufu mbaya ya mwili.

Kulingana na wataalamu, zabibu ina vitamini C mara nne zaidi kuliko vinjwaji vingi vya juisi wakati oksidi pia hupatikana ndani yake.

Zabibu pia inaweza kutumika kwa madhumuni ya matibabu katika siku zijazo.

Vinavyopatikana ndani ya tunda la zabibu vinafanyiwa majaribio ili kuona jinsi vinaweza kutumika kutibu shinikizo la damu na matatizo ya akili.

Profesa Aidan Cassidy katika Chuo Kikuu cha Malkia huko Belfast amefanya utafiti ikiwa wanaume wanaweza kutumia zabibu nyeusi kutibu tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Anasema kuwa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume husababishwa na mtiririko wa damu usiofaa.

'Anthocyanin, flavinoid zinazopatikana katika zabibu nyeusi (ambazo hupatia tunda rangi ya zambarau), huboresha mtiririko wa damu,' anasema.

Hii huifanya mishipa ya damu kunyumbulika na kufunguka.'

Uchunguzi wa kina wa miaka 10 wa wanaume zaidi ya 25,000 uligundua kwamba wale waliokula matunda ya anthocyanin au zabibu nyeusi mara tatu au zaidi kwa wiki walikuwa na uwezekano wa asilimia 19 chini ya kupata tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Tunda hili la zabibu pia lina manufaa meningine mwilini.

Utafiti mwingine pia ulionyesha kuwa zabibu nyeusi inaweza kusaidia kuondoa harufu mbaya ya mwili.

"Ikiwa una zaidi ya miaka 45, unatoa gesi maalum kutoka kwa ngozi yako ambayo watu huita", anasema Williams.

Kadiri mwili unavyozeeka, usawa kati ya ‘free radicals na antioxidants’ katika mwili wako unaweza kutoa gesi zinazotolewa kupitia ngozi.

Ingawa utafiti huo ulikuwa mdogo, ukihusisha watu 14 pekee wenye umri wa zaidi ya miaka 55, uligundua kuwa ulaji wa zabibu za unga kwa siku saba ulipunguza gesi kwa asilimia 25.

"Ningependeza sana kuona ikiwa unaweza kupata matunda hayo, lakini kuna uwezekano mkubwa kwamba ni kutokana na athari za antioxidant (ya zabibu)," anasema Mark Williams. Harufu kama hiyo hutolewa.'

Kwa upande mwingine, Williams anasema kuwa kupata zabibu nyeusi inaweza kuwa ghali, kwa hivyo sio suluhisho pekee kwa watu wengi. Wala si dawa ya kipekee kwa matatizo mengine.

'Nadhani bado tunahitaji kuwa makini na madai yetu kwamba ni nzuri kwa kupoteza uzito. Sio dawa ya kidonge ambacho kitasuluhisha shida zako zote.'

Williams pia anaongeza kuwa utafiti mwingi uko katika hatua za awali na majaribio marefu yanahitajika. Basi tahadhari na wale wanaodai kuwa hii ni tiba ya muujiza.

"Ninasimamia na kile tulichopata, kwa mfano, tuna data ambayo haifai kwa watu wa asili ya Kusini-Mashariki mwa Asia. Kwa hiyo bado kuna mengi ya kujifunza na kuzingatia.'


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved