logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ndege ya KDF yaanguka Baringo

Abiria hao walikuwa wakielekea Nairobi kutoka kazini wakati chopa hiyo ilipopata changamoto

image

Habari20 July 2023 - 14:23

Muhtasari


  • Abiria hao walikuwa wakielekea Nairobi kutoka kazini wakati chopa hiyo ilipopata changamoto za kiufundi na kuanguka.

Ndege ya Kenya Airforce iliyokuwa na abiria imeanguka dakika chache baada ya kupaa katika eneo la Bonde la Ufa.

Katika taarifa iliyotolewa Alhamisi, Julai 20, Vikosi vya Ulinzi vya Kenya vilithibitisha kuwa wafanyakazi na abiria wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo walinusurika.

Abiria hao walikuwa wakielekea Nairobi kutoka kazini wakati chopa hiyo ilipopata changamoto za kiufundi na kuanguka.

Iliripotiwa kuwa chopa hiyo ya kijeshi, iliyotambuliwa kama helikopta ya Fennec, haikuchukua muda mrefu angani baada ya kupaa.

"Jioni ya leo, helikopta ya Jeshi la Wanahewa la Kenya, Fennec, ilipokuwa ikiruka kutoka uwanja wa Chemlingot kuelekea Nairobi, iligonga mti na kuanguka," KDF ilisema.

Vikosi vya Ulinzi vya Kenya pia viliwahakikishia wananchi kwamba wafanyakazi wao watapata ahueni kamili kwa vile waliohusika katika ajali hiyo walikuwa wakipata matibabu ya kutosha.

"Abiria wote walishuka salama na wako katika hali shwari," Jeshi la Ulinzi la Kenya lilithibitisha katika taarifa iliyotumwa kwa vyumba vya habari.

 

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved