logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanamume amuua mwenzake kwa kutomlipa deni ya Ksh.50 Turkana

Juhudi zake ziliambulia patupu kwani umati huo wenye hasira ulimkamata na kumpiga mawe hadi kufa.

image

Habari04 August 2023 - 11:30

Muhtasari


  • Mtu aliyechomwa kisu alifariki mara baada ya tukio hilo, huku muhusika akikimbia baada ya kundi la watu kuanza kukusanyika eneo la tukio

Wanaume wawili wa umri wa makamo walipoteza maisha yao Alhamisi huko Lokichar, Kaunti ya Turkana, kufuatia visa viwili vinavyohusiana vilivyohusishwa na deni ambalo halijalipwa.

Mmoja wa waathiriwa anasemekana kumdunga kisu mwingine kifuani kwa kukosa kulipa deni la Ksh.50 lililoripotiwa kupatikana kutokana na mauzo ya kuku.

Mtu aliyechomwa kisu alifariki mara baada ya tukio hilo, huku muhusika akikimbia baada ya kundi la watu kuanza kukusanyika eneo la tukio

Juhudi zake ziliambulia patupu kwani umati huo wenye hasira ulimkamata na kumpiga mawe hadi kufa.

"Alijaribu kutoroka lakini umati wenye hasira ulimfuata na kumpata. Kisha wakampiga kwa mawe hadi kufa," shahidi aliyeshuhudia aliambia runinga ya Citizen.

Miili ya wawili hao imehamishiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Lodwar.

Wazee wa eneo hilo wamelaani kisa hicho huku wakiwataka vijana kutosababisha vurugu wakati wa kusuluhisha tofauti zao.

 

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved