logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanamume afariki wakati wa mazoezi ya kuchukuliwa kwa makurutu wa kujiunga KDF

Francis alifariki akiwa na umri wa miaka 25.

image
na Radio Jambo

Habari06 September 2023 - 08:22

Muhtasari


• Baada ya kuzirai, Francis alikimbikwa katika hospitali ya rufaa ya Kerugoya ambapo alifariki jioni ya siku hiyo, ripoti hiyo ilisema.

Mwanamume aliyeanguka na kuzirai katika iwanja wa Kirinyaga wakati wa mazoezi ya uteuzi wa kujiunga na jeshi la Kenya, KDF ameripotiwa kufariki akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya kaunti hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti ya Citizen, kijana huyo aliyetambuliwa kwa jina Francis alianguka chini na kuzirai wakati wa kumaliza mzunguko wa mwisho wa mbio katika uwanja huo.

Waliokuwa wanawania kuteuliwa kama makurutu wapya wa KDF walikuwa ni sharti washiriki mazoezi mepesi ili kujiweka katika nafsi nzuri ya kuteuliwa.

Baada ya kuzirai, Francis alikimbikwa katika hospitali ya rufaa ya Kerugoya ambapo alifariki jioni ya siku hiyo, ripoti hiyo ilisema.

“Alikuwa akikimbia na waajiri wengine kabla ya kupata matatizo na alifariki baada ya kupelekwa katika Hospitali ya Kerugoya. Kwa sasa, mwili wake umehifadhiwa katika Mazishi ya Kibugi huko Kutus ukisubiri uchunguzi wa maiti ili kubaini kilichosababisha kifo chake,” kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Kirinyaga Mashariki Millicent Ochuka alinukuliwa na Citizen.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 25 alitajwa na familia yake kama mwadilifu ambaye walikuwa na matumaini kwamba angetimiza ndoto yake ya muda mrefu ya kulitumikia taifa ndani ya magwanda ya KDF.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved