Tiba ya HIV iko tayari kwa majaribio

Kwa sasa kuna karibu watu milioni 40 wanaoishi na VVU duniani.

Muhtasari

•Majaribio ya tiba ya virusi vya ukimwi (VVU) yanatarajiwa kuanza nchini Denmark kabla ya mwisho wa mwaka.

•Mwaka ujao, pamoja na Denmark, majaribio ya dawa hiyo pia yataanza huko Melbourne, Australia.

Image: BBC

Majaribio ya tiba ya virusi vya ukimwi (VVU) yanatarajiwa kuanza nchini Denmark kabla ya mwisho wa mwaka, kupata dawa ambayo inaweza kuthibitisha kuwa tiba iliyosubiriwa kwa muda mrefu ya virusi hivyo vya ugonjwa wa Ukimwi.

Matokeo ya majaribio ya awali ya maabara yaliyofanywa na timu mbili za wanasayansi wa Australia kwa ushirikiano na wenzao kutoka Denmark yanatia moyo kuhusu matumaini ya kupata dawa.

Utafiti wa Australia unaonyesha kwa hakika kwamba dawa ya Oncologic venetoclax ina uwezo wa kuchunguza "seli" katika mwili wa binadamu ambazo zinaathiriwa vibaya na virusi.

Mwaka ujao, pamoja na Denmark, majaribio ya dawa hiyo pia yataanza huko Melbourne, Australia.

Wakati huo huo, vidonge vyenye jina la kibiashara la VENCLEXTA vilitengenezwa awali ili kupambana na saratani ya damu.

Ilithibitishwa nchini Marekani mnamo 2016 na tangu wakati huo, kulingana na madaktari, tayari imesaidia maelfu ya wagonjwa wa saratani.

Kwa sasa kuna karibu watu milioni 40 wanaoishi na VVU duniani.

Uchunguzi na hatimaye utumiaji wa dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo unawezesha kuzuia kuongezeka kwa virusi vya ukimwi , hali inayozuia uharibifu wa kinga ya mwathiriwa mara moja.

Wakati mtu anapotumia dawa mara kwa mara , mwathiriwa pia huwacha kuwa hatari kwa wapendwa wake – lakini yeye mwenye haponi kabisa.

Unapowacha kutumia dawa kila siku makali ya ugonjwa huo hurudi.