logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Gavana wa Kericho, naibu wake wazika tofauti zao baada ya onyo la Gachagua

Naibu wake Mhandisi Fred alisema wametatua suala lao na ni wakati sasa wa kuwahudumia wakazi.

image

Habari11 September 2023 - 15:34

Muhtasari


  • Ijumaa iliyopita, Naibu Rais Rigathi Gachagua aliambia gavana na naibu wake kusahau tofauti zao la sivyo wajihatarishe kupigiwa kura.

Gavana wa Kericho Eric Mutai na naibu wake Fred Kirui walizika tofauti zao kabla ya ziara ya Rais William Ruto katika kaunti hiyo kwa sherehe za Mashujaa Day.

Wawili hao baada ya mkutano uliofanyika Jumatatu walijutia muda uliopotea tangu uchaguzi mkuu uliopita.

Katika mkutano uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mafunzo cha Kericho, wawili hao waliapa kutojihusisha na vita vya maneno ambavyo vimekaribia kukomesha shughuli za kaunti.

Ijumaa iliyopita, Naibu Rais Rigathi Gachagua aliambia gavana na naibu wake kusahau tofauti zao la sivyo wajihatarishe kupigiwa kura.

DP alisema Kericho ambayo ni makazi ya rais na ngome ya kisiasa ilikuwa hali ya kuvunjika moyo na aibu kutokana na vita vya maneno visivyoisha kati ya wawili hao.

Mbunge wa Ainamoi katika bunge la kitaifa Benjamin Langat na mbunge wa kike wa kaunti hiyo Beatrice Kemei walishinikiza maridhiano ya gavana na naibu wake.

"Hatutahusika tena katika vita vya maneno wakati ambapo tunafaa kuwahudumia wakazi wa kaunti," gavana huyo alisema.

Naibu wake Mhandisi Fred alisema wametatua suala lao na ni wakati sasa wa kuwahudumia wakazi.

"Tumepoteza wakati wa maana tangu uchaguzi mkuu uliopita. Wakaazi wa kaunti walitupa mamlaka ya kuwaongoza lakini kwa mwaka jana imekuwa wakati wa kutaja majina miongoni mwa wafuasi wetu kutokana na tofauti zetu za kisiasa," Kirui alisema.

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved