Mwanafunzi wa darasa la nane afariki katika tukio linaloaminika kuwa la kujitia kitanzi ndani ya kanisani huko Homa Bay.
Polisi katika eneo la Rachuonyo Mashariki, Kaunti ya Homa Bay wanachunguza kisa ambapo mwili wa msichana wa miaka 16 ulipatikana katika kanisa moja katika kijiji cha Ogenga ukining'inia kwa kamba karibu na shule yake.
Kulingana na naibu chifu wa eneo la Kasewe, Dickson Samba, mwanafunzi huyo aliondoka nyumbani siku ya Jumanne , lakini mamake alimpata saa moja baadaye.
Bado haijabainika nini kilichochea msichana huyo kujiua, polisi wameanzisha uchunguzi.