Gavana wa Siaya James Orengo amemteua aliyekuwa mbunge maalum Prof Jacqueline Adhiambo Oduol kwa wadhifa wa waziri wa kaunti (CEC).
Orengo amemteua mbunge huyo wa zamani katika serikali yake kama waziri wa maji, Usafi wa Mazingira, Mabadiliko ya Tabianchi na Maliasili. Jina la Prof. Oduol ni miongoni mwa walio kwenye orodha ya waliopendekezwa ambayo gavana huyo aliwasilisha kwa Bunge la Kaunti kwa uidhinisho.
Iwapo itaidhinishwa Oduol atasimamia idara ya maji ambayo imekuwa wazi baada ya Dkt Julie Onyango kuondoka baada ya kufurushwa na bunge la kaunti kwa madai ya utovu.
Wengine ambao wako kwenye orodha ya gavana Orengo ni pamoja na Jacktone Odinga (Bajeti na mipango), Ajuul Okoth Kevin (Nishati na Uchukuzi), Samuel Omondi Owino (Afya), Judith Oyugi (Maji na Usafi) na Adongo Elizabeth Atieno. (Kilimo).
Walioteuliwa katika nyadhifa za Maafisa Wakuu ni pamoja na Oliech Michael Ombambo (Biashara na Maendeleo ya Viwanda) na hatimaye Dkt, Nicholas Kut Ochogo (Vijana, jinsia na huduma za kijamii).
Walioteuliwa watapigwa msasa na bunge na kuidhinishwa au kukataliwa.