logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mkurugenzi wa fedha wa Nairobi Hospital alidungwa mara 25-Uchunguzi wa maiti wafichua

“Tulipiga hesabu na kukuta alikuwa na majeraha 25 ya kuchomwa kisu.

image

Habari17 September 2023 - 04:00

Muhtasari


  • Alisema hakukuwa na majeraha ya ulinzi akimaanisha mtu huyo alikuwa amelala huku akichomwa kisu.
  • Mshambuliaji hakuiba chochote kutoka kwa nyumba ya marehemu, polisi walisema.

Mkurugenzi wa fedha wa Nairobi Hospital Erick Maigo alikuwa na majeraha 25 ya kuchomwa visu na kusababisha kifo chake, uchunguzi wa maiti unaonyesha.

Uchunguzi wa upasuaji wa maiti ambao ulifanywa katika Jumba la kuhifadhi maiti la Lee mnamo Jumamosi ulifichua baadhi ya viungo muhimu vilinyakuliwa na visu kwenye shambulio hilo.

“Tulipiga hesabu na kukuta alikuwa na majeraha 25 ya kuchomwa kisu. Hili lilisababisha kuvuja damu nje na ndani,” akasema mtaalamu mkuu wa serikali Dkt Johansen Oduor

 

Alisema hakukuwa na majeraha ya ulinzi akimaanisha mtu huyo alikuwa amelala huku akichomwa kisu.

Mshambuliaji hakuiba chochote kutoka kwa nyumba ya marehemu, polisi walisema.

Maigo, 36 alipatikana Ijumaa asubuhi akiwa ameuawa katika nyumba yake eneo la Woodley, Nairobi. Mwili wa Maigo ulipatikana na visu 25 dakika chache baada ya kuuawa mwendo wa saa kumi na mbili asubuhi, polisi walisema.

Mshambulizi wake, mwanamke ambaye labda alikuwa amelala nyumbani kwake alitoroka dakika chache kabla ya polisi kufika.

Hakuna aliyekamatwa hadi sasa. Polisi walikuwa wamehesabu majeraha 16 ya visu kwenye eneo la tukio lakini uchunguzi wa maiti ulithibitisha kuwa walikuwa 25.

"Hii iliendeshwa na hasira au kitu kingine. Bado hatujajua,” afisa mmoja anayefahamu uchunguzi huo alisema

Familia yake ilihudhuria zoezi la upasuaji wa maiti Majirani katika ghorofa ya Woodley Annex walisema walimsikia Maigo akiugua kwa maumivu. Waliamua kuuendea mlango wake na kuugonga ndipo akakutana na mwanamke mmoja ambaye aliwajulisha kuwa kila kitu kilikuwa sawa na alikuwa anatafuta funguo ili afungue.

Mwanamke huyo alichungulia dirishani akidai kuwa hakuweza kupata ufunguo. Majirani walimsikia Maigo akiwa bado anaugulia maumivu na kutafuta msaada.

Bibi aliyekuwa ndani ya nyumba hiyo alikataa kufungua na kuwafanya majirani kuwatahadharisha usalama katika boma hilo. Waliwaomba wanausalama wasiruhusu mtu yeyote kutoka katika nyumba hiyo kuondoka.

Kulingana na polisi, walikimbilia katika kituo cha polisi cha Kibra ambapo walitoa ripoti ya shughuli za kutiliwa shaka katika nyumba hiyo.

Wakati polisi walipofika eneo la tukio, walimkuta mwanamke huyo alipatikana hayupo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved