logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanamume arejea nyumbani baada ya kutoweka miaka 51 Homabay

Lakini badala yake alihamia Mombasa ambako alikaa muda wote.

image

Habari18 September 2023 - 11:01

Muhtasari


  • Mzee Odongo alisema uamuzi wake wa kutoweka nyumbani ni baada ya kutofautiana na kakake ambaye kwa sasa ni marehemu.

Kijiji kimoja katika Kaunti Ndogo ya Homa Bay kinasherehekea kurejea kwa mzee wa miaka 81 ambaye alikuwa ametoweka kwa miaka 51 baada ya kutoweka nyumbani mnamo 1972. Joseph Odongo aliondoka nyumbani kwake katika kijiji cha Riwa, eneo la Kanyada Magharibi alipokuwa na umri wa miaka 30.

Hii ilikuwa baada ya kutofautiana na baadhi ya wanafamilia wake.

Katika kijiji hicho, hakuna mtu chini ya miaka 60 aliyeweza kumtambua aliporudi nyumbani kwani kila aliyezaliwa baada ya kuondoka alisikia habari zake tu lakini hakuwahi kumuona.

Mzee Odongo alisema uamuzi wake wa kutoweka nyumbani ni baada ya kutofautiana na kakake ambaye kwa sasa ni marehemu.

Aliwaambia wanafamilia wachache kwamba alikuwa akienda Sikri beach ambayo iko kilomita chache kutoka nyumbani kwake.

Lakini badala yake alihamia Mombasa ambako alikaa muda wote.

Kwa kuwa njia hiyo ya mawasiliano ilikuwa shida wakati huo, ilikuwa ngumu kumtafuta. Familia yake iliamua kwamba huenda alikufa.

Dada yake Matasia Akelo, mwenye umri wa miaka 90 hata hivyo alikuwa na mawazo tofauti. Kila mara aliomba kwamba mzee Odongo arudi nyumbani.

Baada ya kuungana tena, Mzee Odongo aliambia familia yake kwamba amekuwa akiishi Likoni, Kaunti ya Mombasa, ambako alikuwa ameajiriwa kama mlinzi.

Chifu wa eneo la Kanyada Magharibi Kenneth Achieng alisema mwanamume huyo alitembea hadi afisi yake iliyoko Kabunde kutafuta usaidizi kabla ya kuunganishwa na familia yake.

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved