logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Elon Musk: Watumiaji wa X huenda wakaanza kutoa malipo ili kutumia jukwaa hilo,

Tangu achukue umiliki wa Twitter Musk ametafuta kuhamasisha watumiaji kulipia huduma iliyoboreshwa

image
na Davis Ojiambo

Habari19 September 2023 - 04:34

Muhtasari


  • • Ingawa kuna faida ya kifedha kwa kampuni hiyo kutoza watumiaji, Bw Musk alisisitiza kuwa kupata watu wa kulipia huduma hiyo kunalenga kukabiliana na roboti.

Elon Musk amependekeza kuwa watumiaji wote wa X, ambayo zamani iliitwa Twitter, wanaweza kulipa ili kufikia huduma za mtandao huo

Katika mazungumzo na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, bilionea huyo alisema mfumo wa malipo ndiyo njia pekee ya kukabiliana na utumizi wa akaunti zinazoendeshwa na roboti.

"Tunaelekea kuwa na malipo madogo ya kila mwezi kwa matumizi ya mfumo," bosi wa Tesla na SpaceX alisema.

BBC ilitaka maeleo Zaidi kutoka kwa X lakini bado haijapokea taarifa kutoka kwa kampuni hiyo.

Haijulikani ikiwa haya yalikuwa maoni tu ya pembeni, au ishara ya mipango thabiti ambayo bado haijatangazwa.

Bw Musk amekuwa akisema kwa muda mrefu kuwa suluhisho lake la kuondoa roboti na akaunti ghushi kwenye jukwaa la mitandao ya kijamii ni kutoza ada kwa watumaiji wake.

Tangu achukue umiliki wa Twitter mwaka jana ametafuta kuhamasisha watumiaji kulipia huduma iliyoboreshwa, ambayo sasa inaitwa X Premium.

Hili limefanywa kwa kuwapa watumiaji wanaolipia vipengele zaidi, kama vile machapisho marefu na kuongezeka kwa mwonekano kwenye jukwaa.

Walakini, watumiaji bado wanaweza kutumia X bila malipo.

Ingawa kuna faida ya kifedha kwa kampuni hiyo kutoza watumiaji, Bw Musk alisisitiza kuwa kupata watu wa kulipia huduma hiyo kunalenga kukabiliana na roboti.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved