logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Katibu wa Kudumu Susan Mang’eni ahusika kwenye ajali, mmoja akifariki

Ajali hiyo ilitokea Oktoba 16 katika eneo la Korinda, Kaunti ya Busia.

image
na Davis Ojiambo

Habari17 October 2023 - 07:05

Muhtasari


  • • Polisi walisema mwendesha pikipiki huyo alitangazwa kufariki punde tu alipofika hospitalini.

Mwendesha pikipiki mmoja alifariki papo hapo baada ya pikipiki yake kugongana ana kwa ana na gari la Katibu wa kudumu Biashara ndogo za kadri na ndogo Susan Mang’eni.

Ajali hiyo ilitokea Oktoba 16 katika eneo la Korinda, Kaunti ya Busia. Polisi walisema mwendesha pikipiki huyo alitangazwa kufariki punde tu alipofika hospitalini.

 Kulingana na polisi Mange’eni na dereva wake pia walijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini. Polisi hata hivyo walithibitisha kuwa Mang’eni hakuwa katika hali ya hatari na kwamba anaendelea kupata nafuu. Polisi walisema kilichosababisha ajali hiyo. Amelazwa katika hospitali ya Busia.

Gari la serikali alilokuwa akiisafiriwa Mang’eni liliharibika vibaya na kubururwa hadi kituo cha polisi karibu na eneo la ajali.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved