logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Tuko Azimio kukaa-Karua na kioni waweka wazi

Alipuuza maoni ya kiongozi wa Azimio Raila Odinga aliyoyatoa Jumapili iliyopita

image

Habari23 October 2023 - 14:09

Muhtasari


  • “Kwa sasa, hatuzungumzii hayo bali kuhusu umoja wa watu wa Mlima Kenya. Kalonzo Musyoka ni ndugu yetu.

Kiongozi wa chama cha Narc-Kenya Martha Karua na Katibu Mkuu wa Chama cha Jubilee Jeremiah Kioni Jumatatu walizindua rasmi Kongamano la Uongozi la Kamwene, mkutano ambao wanasema utakuwa wa kukuza masilahi kutoka eneo la Mlima Kenya.

Akiwahutubia wanahabari jijini Nairobi, Karua alisema bado ni wanachama dhabiti wa muungano wa Azimio La Umoja One Kenya - ambapo yeye ni mkuu mwenza - licha ya uvumi kuwa vazi hilo jipya lilikuwa likiashiria kuwepo kwa mpasuko ndani ya upinzani ulipotangazwa kwa mara ya kwanza mwezi Septemba.

Alipuuza maoni ya kiongozi wa Azimio Raila Odinga aliyoyatoa Jumapili iliyopita (na baadaye yakafafanuliwa kuwaalinukul;iwa vibaya) ambayo yalionekana kuwa ni uidhinishaji rasmi wa kiongozi wa Chama cha Wiper Kalonzo Musyoka kama mpeperushaji bendera wa upinzani katika uchaguzi mkuu wa 2027.

“Kwa sasa, hatuzungumzii hayo bali kuhusu umoja wa watu wa Mlima Kenya. Kalonzo Musyoka ni ndugu yetu. Tuko Azimio kukaa lakini bado tuna Kamwene Caucus ya kujadili masuala ya Mlima Kenya,” Karua aliambia wanahabari.

"Yeye (Odinga) aliandika taarifa ya ufafanuzi, lakini hata kama angemuidhinisha, itakuwa ndani ya haki yake. Uidhinishaji haupunguzi kwa vyovyote nafasi za mtu mwingine yeyote ambaye anaweza kutaka kushiriki katika kinyang'anyiro hicho."

Alipoulizwa kuhusu maoni yake kuhusu kisa ambapo Odinga alimuunga mkono Musyoka katika uchaguzi wa 2027, kiongozi huyo wa Narc-Kenya alipuuzilia mbali mazungumzo kama vile ya kukatisha tamaa, akiwaambia wanahabari: “Tulikataa kujihusisha na visumbufu. Wapeleke kwingine, tuko hapa kuzungumzia Kamwene.”

Kumekuwa na ripoti kuwa Karua na Kioni hawajaridhishwa na mazungumzo ya pande mbili yanayoendelea kati ya wabunge wa upinzani na wale wa muungano tawala wa Kenya Kwanza.

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved