logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Hatimaye, Pasta Ezekiel yuko huru baada ya kesi ya kuhusishwa na janga la Shakahola kufungwa

Tusinge simama imara wale ambao wanatutegemea kwa imani yao kesho wangevunjika moyo.

image
na Davis Ojiambo

Habari01 November 2023 - 07:03

Muhtasari


  • • Odero aliachiliwa kuwa huru na mahakama ya Shanzu huko Kilifi huku hakimu akiamuru,mchungaji huyo kurudishiwa dhamana ya Sh milioni 1.5.
  • • "Naagiza  kuachiliwa kwa mhojiwa, Ezakiel Odero.Dhamana ya pesa taslimu ya Ksh 1.5 milioni ambayoilitolewa na mshtakiwa irudishwe mara moja,na faili hili sasa limefungwa,"
Pasta Ezekiel

Mchungaji Ezekiel Odero wa kanisa la  New Life Prayer Center ambaye alishukiwa kuwa mhusika mkuu wa mauaji  ya Shakahola hatimye aliondolewa mashtaka hayo.

Odero aliachiliwa kuwa huru na mahakama ya Shanzu huko Kilifi huku hakimu akiamuru,mchungaji huyo kurudishiwa dhamana ya Sh milioni 1.5.

Timu ya mashtaka iliyokuwa ikiongozwa na Antony Musyoka, iliambia vyombo vya usalama vilivyokuwa vikifanya uchunguzi  kuwa hawakupata ushahidi wowote unaomhusisha Odero na kanisa lake na  kasisi Paul Mackenzie.

"Tunaonelea  kwamba jalada hilo lifungwe katika hatua hii kwa kuwa upelelezi umekamilika na mapendekezo yamo katika majalada ya polisi ambayo yametumwa kwa ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ," alisema.

Kikao cha kusikilizwa kwa kesi hiyo kilichoongozwa na Hakimu Mkuu Joe Omido kilifikia tamati baada ya Hakimui kutoa uamuzi kwamba Odero aachiliwe huru na kwamba dhamana ya pesa taslimu Sh milioni 1.5 ambayo mhubiri huyo alilipa mapema kortini kwa kuachiliwa kwake kwa muda irudishwe.

“Baada ya kutafakari maombi yaliyotolewa jana na wakili wa mwandishi na kutafakari zaidi majibu yaliyotolewa na wakili wa upande wa mashtaka, ambaye amewasilisha taarifa kupitia barua ya Oktoba 30, 2023 na kutafakari kwa ukamilifu rekodi hiyo, naagiza  kuachiliwa kwa mhojiwa, Ezakiel Odero.Dhamana ya pesa taslimu ya Ksh 1.5 milioni ambayoilitolewa na mshtakiwa irudishwe mara moja,na faili hili sasa limefungwa,"alisema jaji Omido.

Mchungaji Ezekiel baada ya kuachiliwa huru alisema kwamba anaichukulia kama kesi kutoka kwa Mungu na kwamba hana kinyongo chochote dhidi ya ofisi ya upelelzi na mashtaka kwa kumchunguza.

"Sidhani kama hii ilimhusu Ezekiel, hii ilihusu kanisa na siku zijazo. Tusinge simama imara wale ambao wanatutegemea kwa imani yao kesho wangevunjika moyo. Lakini kama Mungu aliona tunastahili kupitia mtihani huu, ili kuthibitisha kama tunastahili, tunasema asante Bwana kwa mtihani huu. Ukweli umetuweka huru” alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved