Naibu wa Rais Rigathi Gachagua amemtetea Rais William Ruto baada ya tetesi za kufanya ziara nyingi zaidi nje ya nchi ya kipindi kifupi tangu alipochukua hatamu a uongozi.
Akiwashutumu wakosoaji, Naibu Rais Alhamisi alisema kuwa safari za Rais William Ruto zinaleta manufaa katika miradi mbalimbali ya maendeleo ya nchi.
"Rais kuna wale wanakupigia kelele ati unaenda nchi za Ng’ambo sijui kufanya nini…Tungetaka kuambiwa matunda ya rais kutembea nchi imepatikana , wengine wepata kazi kupitia safari zako "alisema.
Aidha, Gachagua alimtaka Rais Ruto kusafiri zaidi mpaka pale atakpo hakikisha kuwa wakenya wamenufaika zaidi.
Gachagua alisisitiza kuwa Rais alichaguliwa na kupewa mamlaka ya kusaidia Wakenya na kuboresha uchumi wa taifa.
"Ukiona Merekani ni penye Wakenya watafaidika , paa angani na uende,Wanaouliza waje kushuhudia kile ambacho rais anaagiza kwa faida ya wakenya," Gachagua alisema.
"Rais anaenda kazi si kujivinjari,lazima rais atembeee kwa manufaa ya nchi, Rais, nataka nikutie moyo kwa safari zako kwa sababu zimeiweka Kenya kwenye ramani ya dunia," aliongeza.
Siku ya Jumapili, Rais William Ruto alitetea ziara zake tangu ashike wadhifa wauongoi akisema kuwa kila anachofanya ni kwa manufaa ya wakenya ambao wanaghadhabishwa na hali ya uchumi.
Akiongea wakati wa ibada katika kanisa la Uasin Gishu siku ya Jumapili, Ruto alisema ni kupitia safari hizo ambapo ameweza kupata mikataba kadhaa kwa ajili ya nchi.
Alibainisha kuwa ziara yake ya hivi majuzi nchini Saudi Arabia ilimwezesha kupata nafasi za ajira kwa Wakenya 350,000 huku mkataba wa nchi mbili ukitarajiwa kutiwa saini katika muda wa wiki tatu zijazo.