logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Quickmart yasema 94m zilizopotea katika wizi hazitaathiri shughuli zao

Biashara ni salama tuweka bima dhidi ya matukio kama hayo Quickmart yasema

image
na Davis Ojiambo

Habari08 November 2023 - 14:51

Muhtasari


  • •Polisi Jumatatu walianzisha msako wa kuwatafuta walinzi  wawili ambao waliripotiwa kuimba Sh94.9 milioni za kampuni ya 
  • •Quickmart alidokeza zaidi kwamba mamlaka za uchunguzi zimekuwa  zikifanya kazi kwa bidii kutatua suala hilo.

Kampuni inayomiliki Maduka ya jumla ya Quickmart imetowa hakikisho kwa wateja wake kuwa wizi wa hivi majuzi wa Shilingi milioni 94 hautaathiri shughuli za kawaida za maduka hayo. 

"Tungependa kuhakikishia  wateja na washirika wetu kwamba tukio hilo la wizi halitavuruga shughuli zetu za kila siku," ilisema taarifa hiyo. "

Tunasalia kujitolea kuwahudumia wateja wetu na washirika kwa uadilifu na kujitolea kwa vyovyote kurekebisha tukio hilo walisema.

Quickmart ilithibitisha zaidi kwamba kama kampuni inayojulikana, biashara yao iko salama kwasababu wana bima ya kifedha dhidi ya matukio kama hayo.

Aidha walieleza kuwa mamlaka husika zinafanya kazi kikamilifu kuwatia nguvuni washukiwa.

Polisi siku ya Jumatatu walianzisha msako wa kuwatafuta walinzi  wawili walioripotiwa kuitoroka na shilingi milioni 94.9 zilizo kuwa zinasafirishwa kwa benki moja jijini Nairobi.

Pesa hizo zilitoka kwenye  kampuni ya ulinzi katika eneo la Industrial Area na zilipaswa kuwasilishwa kwa benki moja katikati mwa jiji.

Wawili hao waliokuwa kwenye gari la kampuni hiyo walikuwa wamefika kwenye chumba hicho kama ilivyoratibiwa lakini waliondoka bila kusindikizwa na polisi.

Polisi walisema waligundua gari lililokuwa na pesa halikuwepo dakika chache baada ya kuripotiwa kutoweka.

Gari hilo lilipatikana likiwa limehegeshwa kwa  njia huku  washukiwa wakiwa wametoweka na pesa.

Maafisa  wa polisi walitembelea eneo la tukio na kubaini kuwa wawili hao walitoroka ndani ya gari lililokuwa likisubiri.

Polisi walisema tukio hilo lilikuwa jipya na linaonekana kuwa jama iliyopagwa.

Maafisa ambao walipaswa kusindikiza gari hilo  iliyohusika katika wizi huo walihojiwa kama sehemu ya uchunguzi wa tukio hilo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved