logo

NOW ON AIR

Listen in Live

NSSF yatangaza nafasi zaidi ya 300 za kazi

Watu wanaovutiwa wanashauriwa kuwasilisha wasifu kazi katika makao ya azina hiyo kabla ya tarehe 11 Desemba 2023.

image
na Davis Ojiambo

Habari21 November 2023 - 13:27

Muhtasari


  • • Katika notisi, kuna nafasi 336 ambazo hazina hiyo inataka watu wenye kutuma maombi ya kazi
  • • “Hazina ya Kitaifa ya malipo ya uzeeni ina vituo vya kutolea huduma vilivyoenea kote nchini na inalenga kuimarisha uwezo wa rasilimali  ili kutimiza wajibu wake wa kutoa huduma kwa Wakenya wote,”

Hazina ya kitaifa ya malipo ya uzeeni NSSF imetangaza nafasi za kazi katika sekta mbalimbali.

Katika notisi, kuna nafasi 336 ambazo hazina hiyo inataka watu wenye kutuma maombi ya kazi.

“Hazina ya Kitaifa ya malipo ya uzeeni ina vituo vya kutolea huduma vilivyoenea kote nchini na inalenga kuimarisha uwezo wa rasilimali  ili kutimiza wajibu wake wa kutoa huduma kwa Wakenya wote,” ilisema notisi hiyo.

Baadhi ya nafasi hizo ni pamoja na meneja wa Mkoa (6), meneja msaidizi (19), meneja wa tawi (15), afisa mkuu mwandamizi (28) mhasibu (24), afisa  wa usalama (2),msimamizi wa rekodi (2), afisa mkuu (78). ) msimamizi mkuu wa wakufunzi (46) miongoni mwa nafasi nyinginezo.

Watu wanaovutiwa wanashauriwa kuwasilisha wasifu kazi katika makao ya azina hiyo kabla ya tarehe 11 Desemba 2023.

Takwimu kutoka kwa ripoti ya Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu ya Kenya ya Ripoti ya Wafanyakazi wa Kila Robo ya Oktoba-Desemba 2022 ambayo ilitolewa Februari inaonyesha ukosefu wa ajira nchini Kenya ulipungua hadi 960,001 ambayo ni  (asilimia 4.9) katika kipindi cha Desemba 2022 kutoka 1,055,816 ambayo ni  (asilimia 5.6) katika robo hiyo hiyo  ya mwaka wa 2021.

Serikali imesema itatoa nafasi za kazi kwa vijana.

Wiki iliyopita, Waziri wa Utumishi wa Umma na Usimamizi wa Uwasilishaji Moses Kuria alisema wizara yake hivi karibuni itazindua tovuti ya 'Jobo Bila Connection initiative'.

Waziri huyo alisema tovuti hiyo itawasaidia Wakenya kutuma maombi ya kazi katika sekta ya umma bila kujali asili zao.

"Katika sekta ya umma, tutaongoza kutoka mbele. Hivi karibuni tutatengeneza tovuti ya Wakenya wote kutuma maombi ya kazi katika sekta ya umma bila kujali asili yao iliyopewa jina la Jobo Bila Connection initiative," alisema.

"Suala la ukosefu wa ajira kwa vijana linapaswa kuwa wasiwasi kwetu sote kwa sababu hatuko salama hadi pale sisi sote tutakuwa salama" alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved