Wakenya sasa wanasababu ya kutabasamu baada ya serikali kutangaza kupungua kwa bei ya umeme.
Kulingana na Wizara ya Nishati, bei za umeme kwa watumiaji wote zitapungua kwa Ksh.3.44 kwa kila uniti.
Katibu Mkuu wa Kawi Alex Wachira amehusisha mabadiliko hayo na kushuka kwa kiwango cha ubadilishaji wa fedha za kigeni.
"Mabadiliko ya ubadilishaji wa fedha za kigeni yalipungua kutoka Ksh.6.46 kwa kilowati hadi Ksh.3.22 kwa kilowati kutokana na kupungua kwa jumla ya malipo ya ubadilishaji wa fedha za kigeni yaliyofanywa Januari," alisema Jumatano.
PS Wachira pia alihusisha mabadiliko ya bei na punguzo la chini la Gharama ya Nishati ya Mafuta ambayo ilishuka kwa senti 19.
Watumiaji wa malipo ya awali wataona mabadiliko mara moja lakini wale malipo ya baada ya matumizi wataona mabadilko mwezi huu wa februari.