logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Otile Brown afunguka kwa nini alikosa kumuoa Nabayet, kwa nini amekuwa single muda mrefu

Amesema alifanya jitihada za kwenda Ethiopia na kujaribu kumshawishi arudi lakini jitihada zake hazikuzaa matunda.

image
na Radio Jambo

Habari24 February 2024 - 06:56

Muhtasari


•Otle alisema kuwa ilimhitaji ujasiri mkubwa kuweza kufanya wimbo huo unaozungumzia misukosuko ya uhusiano wake uliovunjika.

•Amesema alifanya jitihada za kwenda Ethiopia na kujaribu kumshawishi arudi lakini jitihada zake hazikuzaa matunda.

Mwanamuziki mahiri wa Kenya Jacob Obunga almaarufu Otile Brown amekiri kuwa wimbo ‘Dear X’ katika albamu yake mpya umeimbwa kwa ajili ya mpenzi wake wa zamani Nabayet almaarufu Nabbi.

Akizungumza kupitia ukurasa wake wa Instagram siku ya Ijumaa jioni, mwimbaji huyo mzaliwa wa Pwani alisema kuwa ilimhitaji ujasiri mkubwa kuweza kufanya wimbo huo unaozungumzia misukosuko ya uhusiano wake uliovunjika.

Aliendelea kuongea jinsi alivyokuwa akimpenda mrembo huyo kutoka Ethiopia na jinsi alivyodhamiria kufunga ndoa rasmi naye.

“Nilimpenda sana Muethiopia, niltaka sana kumuoa. Ila kisa nilimuumiza sana kipindi cha nyuma alinikataa mara kadhaa,” Otile Brown alisema.

Alikiri kwamba baada ya kumuumiza Nanbi na kupelekea agure Kenya, alifanya jitihada za kwenda Ethiopia na kujaribu kumshawishi arudi lakini jitihada zake hazikuzaa matunda.

"Lakini ata mimi pia sikumpambania sana maana nilihisi amebadilika sio yule Muethiopia niliyemjua, zile heartbreak na long distance zilimkatisha tamaa.. I had to take the L and let go," alisema.

Mwimbaji huyo mwenye talanta kubwa alisema kutengana na Nabayet kulimuathiri sana hadi akapata ugumu wa kuingia katika mahusiano mapya.

“Huo uamuzi ulinitesa sana, nikakaa kipindi kirefu maana nilihisi hakuna mtu anayenielewa kama yeye na nilikuwa na uwoga kuwa huenda sitawahi kumpata mtu kama yeye maisha yangu yote,” alisema.

Hata hivyo alitumia fursa hiyo kufichua kuwa hatimaye ameweza kuingia kwenye uhusiano mwingine na kuwataka watu kumheshimu mpenzi wake.

"Kwa ndugu zangu wakubwa na dada, mama na pops kwenye dms zangu, daima upendo na heshima kwake," alisema.

Mwimbaji huyo mzaliwa wa pwani alithibitisha kutengana na mrembo huyo kutoka Ethiopia mnamo Januari 2022 baada ya kutoka naye kwa karibu miaka mitatu.

Wawili hao waliingia kwenye uhusiano mapema 2019, miezi michache tu baada ya Otile kuachana na sosholaiti maarufu wa Kenya Vera Sidika.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved