logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Vihiga: Mama wa miaka 59 azirai na kufariki wakati wa ibada ya kesha

Polisi waneanzisha uchunguzi dhidi ya tukio hilo.

image
na Davis Ojiambo

Habari17 March 2024 - 03:42

Muhtasari


  • • Mhudumu wa hospitali ya kibinafsi ambaye aliitwa kwenye eneo la tukio alithibitisha kuwa mwanamke huyo alikuwa tayari amefariki.
crime scene 1

Huzuni na vilio vilitanda katika kanisa la Jesus Power, eneo la Sabatia kaunti ya Vihiga baada ya mama mmoja mwenye umri wa miaka 59 kudaiwa kuzirai na kufariki dunia baadae wakati wa ibada ya kesha mapema Jumamosi alfajiri.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka kaunti hiyo, alizimia asubuhi na mapema katika kanisa hilo linalojulikana kwa jina la Jesus Power, huku juhudi za waumini kumsaidia zikishindikana.

Mhudumu wa hospitali ya kibinafsi ambaye aliitwa kwenye eneo la tukio alithibitisha kuwa mwanamke huyo alikuwa tayari amefariki.

Maafisa wa polisi waliarifiwa na kufika eneo la tukio ambapo wameuhamisha mwili wa marehemu hadi chumba cha kuhifadhia maiti.

Aidha chifu huyo alieleza kuwa familia ya marehemu ilithibitisha kuwa mwanamke huyo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Pumu hali inayoshukiwa kusababisha kifo chake.

Mwili wa muumini huyo ulipelekwa katika makafani na uchunguzi kuanzishwa ili kubaini chanzo halisi cha kifo chake.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved