logo

NOW ON AIR

Listen in Live

KPLC yatangaza maeneo yatakayoathirika na kukatizwa kwa stima leo, Jumanne

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Machi 19.

image
na SAMUEL MAINA

Habari19 March 2024 - 04:45

Muhtasari


  • •KPLC ilitangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
  • •Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Nairobi, Kiambu, Uasin Gishu, Nyeri, Kirinyaga, Homa Bay na Kilifi.

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Machi 19.

Katika taarifa ya siku ya Jumatatu jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Nairobi, Kiambu, Uasin Gishu, Nyeri, Kirinyaga, Homa Bay na Kilifi.

Katika kaunti ya Nairobi, maeneo ya Chuo Kikuu cha Kenyatta, Lavington na Westlands yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu za maeneo ya Kiukenda na Kiamumbi katika kaunti ya Kiambu zitaathirika na kukatizwa kwa stima kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Chaka, Karundas, Mbiriri Gitugi Tea Factory katika kaunti ya Nyeri zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Uasin Gishu, sehemu kadhaa za maeneo ya Leseru na Lower Sosian zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.

Katika kaunti ya Kirinyaga, sehemu za maeneo ya Kagumo na Mutira zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Gendia na Simbiri katika kaunti ya Homa Bay zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.

Sehemu kadhaa za eneo la Vipingo katika kaunti ya Kilifi pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved