KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Machi 21.
Katika taarifa ya siku ya Jumatano jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti sita za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Nairobi, Nyeri, Kiambu, Uasin Gishu, Homa Bay, na Kirinyaga.
Katika kaunti ya Nairobi, baadhi ya sehemu za barabara ya General Mathenge na Kasarani Clay City zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu kadhaa za maeneo ya Ndula, Kilimambogo na Ngoliba katika kaunti ya Kiambu zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Baadhi ya sehemu za eneo la Munyaka katika kaunti ya Uasin Gishu pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.
Katika kaunti ya Homa Bay, sehemu kadhaa za maeneo ya Kosele na Karabok zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.
Soko la Kianjiru na la Mururi katika kaunti ya Kirinyaga pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.
Baadhi ya sehemu za maeneo ya Waihara na Kihuri katika kaunti ya Nyeri zitakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.