logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanaume 'apata afueni kubwa' baada ya kupandikizwa figo ya nguruwe

Mzee huyo alipata figo mpya kutoka kwa nguruwe ambayo ilibadilishwa vinasaba ili kupunguza hatari ya kukataliwa kwa kiungo hicho.

image
na SAMUEL MAINA

Habari23 March 2024 - 04:44

Muhtasari


  • •Mzee huyo alipata figo mpya kutoka kwa nguruwe ambayo ilibadilishwa vinasaba ili kupunguza hatari ya kukataliwa kwa kiungo hicho.

Mzee wa miaka 62 anasemekana kupata nafuu na anatakiwa kuondoka hospitalini hivi karibuni, baada ya kupata figo mpya kutoka kwa nguruwe ambayo ilibadilishwa vinasaba ili kupunguza hatari ya kukataliwa kwa kiungo hicho.

Madaktari wa upasuaji wa Marekani wanasema Rick Slayman ni "shujaa halisi" kwa kuwa wa kwanza kujaribu upasuaji huo.

Lengo la mwisho ni kutumia viungo vya wanyama kwa upandikizaji zaidi.

Siku za nyuma, figo za nguruwe ziliwekwa ndani ya ubongo watu waliokufa kwa kama majaribio.

Upasuaji huo wa saa nne, uliofanyika tarehe 16 Machi, "unaashiria hatua kubwa katika jitihada za upatikanaji wa viungo vinavyopatikana kwa urahisi zaidi kwa wagonjwa", Hospitali Kuu ya Massachusetts ilisema katika taarifa.

Bw Slayman alipandikizwa figo ya binadamu katika hospitali hiyo hiyo mwaka wa 2018 baada ya kuwa kwenye matibabu kwa miaka saba kwa sababu figo zake mwenyewe hazikuwa zikifanya kazi ipasavyo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved