logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Bunduki ya OCS iliyoibwa Vihiga yanaswa Nairobi jambazi 1 akipigwa risasi na makachero

Wawili walichana mbuga huku mmoja akisalia na kutaka kupambana nao kabla ya kuuawa.

image
na Davis Ojiambo

Habari10 April 2024 - 07:51

Muhtasari


  • • Majambazi hao watatu baada ya kufumaniwa na polisi na kutakiwa kujisalimisha, wawili walichana mbuga huku mmoja akisalia na kutaka kupambana nao kabla ya kuuawa.
Bunduki iliyoibwa

Makachero wa kitengo cha upepelezi wa uhalifu wa jinai DCI jijini Nairobi wamefanikiwa kuikomboa bunduki aina ya bastola iliyoibwa kutoka kwa OCS wa polisi kaunti ya Vihiga siku kadhaa zilizopita.

 Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyochapishwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii ya DCI, walisema kwamba makachero walikuwa wakiwaandama majambazi ambao wanaaminika kuwasumbua wananchi kwa kutumia silaha kali.

Baada ya makabiliano makali, polisi walifanikiwa kuwaua majambazi wawili katika mtaa wenye shughuli nyingi wa Kasarani na kuinasa bastola hiyo ambayo baadae ilikuja kutambulika kuwa ni ile iliyoibwa kutoka kwa OCS huko Vihiga, Magharibi mwa Kenya.

“Bunduki iliyoibiwa kwa nguvu kutoka kwa Afisa Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Vihiga wakati genge la wahalifu lilipomvamia alipokuwa akishika doria mnamo Desemba 21, 2023 imepatikana Mwiki, kaunti ndogo ya Kasarani.”

“Mwanachama mmoja wa genge hilo ambaye bastola hiyo ilipatikana naye pia aliuawa baada ya kuthubutu kurushiana risasi na timu ya Operesheni ya DCI iliyokuwa ikiwafuata,” sehemu ya ripoti ya DCI ilisoma.

Ili kupata bunduki hiyo, genge hilo katili lilimvizia Inspekta Mkuu alipokuwa akiegesha gari lake katika soko la Vihiga la Majengo, na kumshukia kwa majambia na kumwacha wakidhani amefariki. Kisha wakatoweka na bastola yake ikiwa na risasi 15.

Baada ya kufuatiliwa kwa siku kadhaa, maafisa wa upelelezi kutoka Kurugenzi ya Uendeshaji ya DCI walijibu haraka ripoti ya kijasusi iliyopokelewa kupitia nambari ya simu ya #FichuakwaDCI na mpiga simu ambaye jina lake halikutajwa ambaye aliripoti kuona gari la kutiliwa shaka likiwa na watu watatu waliojihami katika shamba la KU huko Mwiki.

Majambazi hao watatu baada ya kufumaniwa na polisi na kutakiwa kujisalimisha, wawili walichana mbuga huku mmoja akisalia na kutaka kupambana nao kabla ya kuuawa.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved