Aliyekuwa mtangazaji wa KTN News Michael Oyier amefariki.
Oyier alifariki alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali moja jijini Nairobi.
Kulingana na rafiki wa familia, alisema Oyier alianguka katika nyumba yake Lavington jijini Nairobi mnamo Jumatano Aprili 17.
Hii ilikuwa baada ya kulalamika kuhusu maumivu makali ya kichwa.
Madaktari hawakueleza ni nini walichobaini kuwa sababu ya maumivu ya kichwa.
Uchunguzi wa maiti umepangwa kubaini sababu ya kifo cha mtangazaji huyo.
Oyier alijitosa katika PR baada ya kuondoka KTN.
Alicheza pia kama MC katika hafla kadhaa.
Wanahabari Maina Kageni na Carol Radull walimuomboleza Oyier kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii.
Maneno ya Maina yalisomeka, "Tumepoteza legendari. Asante kwa kila kitu Michael Oyier... mmoja wa watangazaji bora sana wa habari ambao nimewahi kuwafahamu.... mfano wa kweli wa kujitolea, nidhamu na kutia moyo!!!! wanahabari wote na familia (Peter, Paul, Olga) na marafiki Rest In Peace Michael Oyier....."
Carol kwa upande wake aliandika, "Habari mbaya zaidi kuwahi kutokea. Aliyekuwa mtangazaji wa KTN na Kiss100 News Michael Oyier alifariki alipokuwa akipokea matibabu."