logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Karen Nyamu afurahia AI ikifanya video yake akitumbuiza kama msanii kwa umati wa mashabiki

Mashabiki wake walimuasa kuchukua fursa hiyo na kujiongeza kwa Sanaa kando na siasa.

image
na Radio Jambo

Habari23 April 2024 - 12:25

Muhtasari


โ€ข โ€œMnanizoea sanaโ€ฆna hapa nyuma mmenifanyia udhalimu,โ€ Nyamu alinukuu video yake ya AI alipokuwa akichangamka kwenye midundo ili kusawazisha.

Karen Nyamu ashangazwa na video yake ya AI

Seneta maalum wa Nairobi, Karen Nyamu ameonesha furaha yake baada ya kukutana na video ya akili mnemba ikimuonesha akitumbuiza kama msanii kwenye jukwaa lililofurikwa na mashabiki.

Nyamu kupitia Instagram yake alipakia video hiyo ikionyesha picha iliyoasisiwa na akili mnemba kama yeye kwenye vazi la samawati na wigi lake akitembea kuelekea jukwaani kabla ya kuanza kutumbuiza akiwarushia mashabiki mikono.

Katika video hiyo, alisema kwa mzaha kuwa watu walikuwa wakimpenda hivyo basi kuhariri video hiyo ili kumfaa. Alibainisha kuwa watu walimtendea isivyo haki huku akiongeza emoji za kucheka mwishoni.

“Mnanizoea sana…na hapa nyuma mmenifanyia udhalimu,” Nyamu alinukuu video yake ya AI alipokuwa akichangamka kwenye midundo ili kusawazisha.

Mashabiki wake walimuasa kuchukua fursa hiyo na kujiongeza kwa Sanaa kando na siasa.

Haya hapa ni baadhi ya maoni ya mashabiki wake kwenye Instagram;

“Ila unaendelea vizuri sana.๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚” k_jeff.

“Mlisema hii Kenya hakuna kupumzika ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚” njeri7664.

“Wow...2027 hivi ndio utakua unajaza kasarani...mungu mbele”micmasmbutu.

Tazama video hiyo hapa;


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoยฉ Radio Jambo 2024. All rights reserved