logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wacheni kujadili mswada wa fedha matangani, Wetangula awambia wabunge

Spika wa bunge alisema kwamba ni kamati za bunge ndizo zilizotoa mswada huo wa bajeti hiyo.

image
na Davis Ojiambo

Habari16 May 2024 - 13:13

Muhtasari


  • • Wetangula aliwataka wabunge kutumia mapumziko ya mwezi mmoja kutafakari Muswada wa kifedha.
  • • Spika wa bunge alisema kwamba ni kamati za bunge ndizo zilizotoa mswada huo wa bajeti hiyo.

Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula amewasihi Wabunge hasa kutoka kwa upinzani kujiepusha na kukosoa Mswada wa Fedha wa 2024 unaopendekezwa katika mazishi na hafla zingine za umma na kusaidia umma kuuelewa vyema.

Kiongozi huyo wa Ford Kenya alizungumza katika eneo bunge la Kabuchai kaunti ya Bungoma siku ya Jumatano wakati wa mazishi ya Mzee Yonah Namuli.

Spika, hata hivyo, aliwataka wabunge kutumia mapumziko ya mwezi mmoja kutafakari Muswada huo wa kifedha akisema kwamba ni kamati za bunge ndizo zilizotoa bajeti hiyo.

"Nyinyi ndio watu mnaokuja na mapendekezo ya bajeti kupitia kamati zenu, tafadhali okoa mateso ya umma na mjiepushe kusimama mbele ya umma na kulalamika sana kuhusu Muswada wa Fedha wa 2024 na ilhali ni nyinyi ndio mnapaswa kutoa mapendekezo ya bajeti," Wetang'ula alisema.

"Wabunge wanapaswa kuketi na kufanya mambo ambayo yanaweza kuwanufaisha watu wa Kenya, wapiga kura wanawategemea na wanawaamini kwa sababu waliwapigia kura."

Wetang’ula aliwaomba wakazi wa Bungoma kuunga mkono serikali ya Rais William Ruto inayoangazia miradi ya maendeleo inayoendelea katika kaunti hiyo.

Wetang’ula alitoa mfano wa ujenzi unaoendelea wa masoko ya Chwele, Chebukube na Kamukunywa unaogharimu Shilingi milioni 300 huko Kimilili.

Pia aliangazia ukarabati wa barabara ya Malala-Kanduyi ambayo alisema itapandishwa hadhi na kuwa ya kiwango cha A ili kukidhi malori makubwa ya kibiashara.

Pia alisema kuwa serikali itatoa Shilingi milioni 25 kwa ajili ya upanuzi na ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Matibabu cha Kenya (KMTC) katika eneo bunge la Kabuchai.

IMETAFSIRIWA NA DAVIS OJIAMBO.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved