logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jinsi ya kuwasilisha maoni kuhusu muswada wa fedha 2024

Wito umetolewa kwa wakenya kuwasilisha maoni yao kuhusu muswada wa sheria ya fedha,2024

image
na Davis Ojiambo

Habari21 May 2024 - 08:53

Muhtasari


  • •Wakenya kuwasilisha maoni yao kuhusu muswada wa sheria  ya fedha kupitia barua pepe
  • •Siku ya mwisho kuwasilisha ni Mei 28,2024 saa kumi na moja jioni.
Bunge la Kenya

Kamati ya Idara ya Fedha na mipango ya kitaifa imetoa wito kwa raia wa Kenya kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kutunga sheria kwa kuwasilisha maoni yao kuhusu mswada mpya wa Fedha wa 2024.Wakenya wanaweza wasilisha maoni yao kwa kuandaa risala,ambayo inaweza wasilishwa kimwili au kutumwa kupitia barua pepe.

Hii itahakikisha kwamba mchakato wa kutunga sheria unakuwa wa uwazi na unazingatia michango ya wadau wote.

'Kwa kuzingatia ibara ya 118[1] [b] ya katiba na kanuni ya kudumu ya 127[3], katibu wa bunge anakaribisha umma na wadau kuwasilisha risala za miswada kwa kamati ya idara ya fedha na mipango ya kitaifa...' taarifa hiyo ya bunge ilisema.

Mswada huo unapendekeza marekebisho katika vipengele kadhaa muhimu vya sheria,ikiwa ni pamoja na sheria ya ushuru wa mapato,sheria ya kodi ya ongezeko la thamani,na sheria ya ushuru wa bidhaa amabayo itaathiri ustawi wa kiuchumi na kifedha wa wakenya wote.

Mswada huo pia utaathiri sheria kama vile sheria ya makazi ya nafuu,sheria ya mafunzo ya viwandani, na sheria ya kulinda data ,ikionyesha athari za maisha na biashara ya wakenya hivo kila mkenya anashauriwa kutoa maoni yake.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved