logo

NOW ON AIR

Listen in Live

KPLC yatangaza maeneo yatakayoathirika na kukatizwa kwa umeme leo Jumanne

Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na  Baringo,Trans Nzoia, Nyeri, Kisii, Nyandarua na Kiambu

image
na SAMUEL MAINA

Habari21 May 2024 - 04:36

Muhtasari


  • •KPLC ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti sita za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
  • •Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na  Baringo,Trans Nzoia, Nyeri, Kisii, Nyandarua na Kiambu

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Mei 21.

Katika taarifa ya siku ya Jumatatu jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti sita za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na  Baringo,Trans Nzoia, Nyeri, Kisii, Nyandarua na Kiambu.

Katika kaunti ya Kiambu, baadhi ya sehemu za maeneo ya Prisons, OJ, BTI, Kidfarmaco na mji wa Kikuyu zitakosa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Kitalale na Kinyoro katika kaunti ya Trans Nzoia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Weru na Murungaru katika kaunti ya Nyandarua zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi unusu alasiri.

Katika kaunti ya Nyeri, sehemu kadhaa za maeneo ya Giakaibei na Naromoru zitakosa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Mogotio Equator na Muya katika kaunti ya Baringo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu kadhaa za mji wa Kisii katika kaunti ya Kisii zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa moja asubuhi na saa kumi na moja jioni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved