logo

NOW ON AIR

Listen in Live

KPLC yatangaza maeneo yatakayoathirika na kukatizwa kwa umeme leo, Jumanne

Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na  Nairobi, Kiambu, Kisumu, Migori, Kisii, Nyeri, na Kirinyaga.

image
na Radio Jambo

Habari28 May 2024 - 04:06

Muhtasari


•Kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

•Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na  Nairobi, Kiambu, Kisumu, Migori, Kisii, Nyeri, na Kirinyaga.

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Mei 28.

Katika taarifa ya Jumatatu jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa moja asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na  Nairobi, Kiambu, Kisumu, Migori, Kisii, Nyeri, na Kirinyaga.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu kadhaa za mtaa wa Njiru zitaathirika na kukatizwa kwa umeme katu ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Toll Station, Murera Coffee, Gikambura na Jambu TV katika kaunti ya Kiambu zitakosa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Eneo la soko ya Chiga katika kaunti ya Kisumu pia litaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa nane alasiri.

Katika kaunti ya Migori, baadhi ya sehemu za maeneo ya Tebesi na Mutinti zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saakumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Kisii, sehemu kadhaa za maeneo ya Kegati na Ekerore zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa moja unusu asubuhi na saa nane unusu mchana.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Muruguru na Marua katika kaunti ya Nyeri zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Githure, Gatitu, Kiamugumo, Kiamutugu, PI na Shunem katika kaunti ya Kirinyaga pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved