logo

NOW ON AIR

Listen in Live

KPLC yatangaza maeneo ambayo yatakosa umeme leo, Jumatano

KPLC ilitangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti tisa za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

image
na SAMUEL MAINA

Habari29 May 2024 - 04:40

Muhtasari


  • •KPLC ilitangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti tisa za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
  • •Kaunti zitakazoathirika ni pamoja na  West Pokot, Kisumu, Migori, Nyamira, Nyeri, Laikipia, Kiambu, Kitui, na Mombasa.

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Mei 29.

Katika taarifa ya siku ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti tisa za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na  West Pokot, Kisumu, Migori, Nyamira, Nyeri, Laikipia, Kiambu, Kitui, na Mombasa.

Katika kaunti ya West Pokot, eneo la Sirikwa Safaris litaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Katolo na Ombeyi katika kaunti ya Kisumu zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa nane mchana.

Sehemu kadhaa za mji wa Migori na Oruba katika kaunti ya Migori zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja asubuhi.

Katika kaunti ya Nyamira, sehemu kadhaa za maeneo ya Ikonge na Mabariri zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi unusu alasiri.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Kiawarigi na Gitunduti katika kaunti ya Nyeri zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa nane mchana.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Gathiuru na Mirera katika kaunti ya Laikipia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa nane mchana.

Katika kaunti ya Kiambu, baadhi ya sehemu za maeneo ya Kihunguro na Rainbow zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Wakati huohuo, sehemu kadhaa za maeneo ya Waita na Kamuongo katika kaunti ya Kitui pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Nyali na Mkomani katika kaunti ya Mombasa pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved