logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Siaya: Mwanamume aingia katika kanisa la Kikatoliki na kunya kwenye sanamu ya Yesu!

Ripoti zaidi zinaonyesha kuwa sanamu hiyo ambayo imekuwa kwenye madhabahu ya kanisa hilo iliripotiwa kutoweka.

image
na Davis Ojiambo

Habari07 June 2024 - 05:19

Muhtasari


  • • “Kisha alijisaidia haja kubwa kwenye sanamu kabla ya kuondoka kanisani. Aliificha sanamu iliyoharibiwa chini ya viti,” polisi walisema.
  • • Mshukiwa huyo anasemekana alikwenda kwenye jumba la juu la sanaa ambapo alikuwa ameificha sanamu hiyo.
  • • Kisha akaonekana akishuka kwenye madhabahu ambako aliichukua sanamu.
Sanamu ya Yesu ukutani

Taharuki na mshangao vilitanda katika kanisa moja kwenye kaunti ya Siaya baada ya mwanamume mwenye umri wa makamo kuripotiwa kuingia kanisani na kunya kinyesi kwenye sanamu ya Yesu Kristo.

Kwa mujibu wa ripoti ya Citizen, tukio hilo la kushangaza lilijiri katika kanisa moja la kikatoliki kwenye kaunti ndogo ya Bondo.

"Kitendo hicho cha kikatili kiliripotiwa katika kituo cha polisi cha Bondo na kasisi wa parokia hiyo," Citizen walimnukuu kamanda wa polisi katika kaunti ya Siaya.

Kamanda wa polisi aliongeza kuwa ripoti zaidi zinaonyesha kuwa sanamu hiyo ambayo imekuwa kwenye madhabahu ya kanisa hilo iliripotiwa kutoweka.

"Baada ya kukagua picha za CCTV, ilibainika kuwa mgeni ambaye alikuwa amevalia shati la mistari nyeusi na nyeupe na suruali nyeusi aliingia katika ukumbi wa kanisa wakati waumini wachache walikuwa wakisali sana," aliongeza.

Mshukiwa huyo anasemekana alikwenda kwenye jumba la juu la sanaa ambapo alikuwa ameificha sanamu hiyo.

Kisha akaonekana akishuka kwenye madhabahu ambako aliichukua sanamu.

“Kisha alijisaidia haja kubwa kwenye sanamu kabla ya kuondoka kanisani. Aliificha sanamu iliyoharibiwa chini ya viti,” polisi walisema.

Juhudi za kumtafuta mshukiwa zilikuwa zinaendelea mpaka wakati taarifa hii inachapishwa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved