logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Pitisheni hiyo budget Haraka! Awaambia wabunge akiwa Meru

Ruto alisema bajeti hiyo ndiyo njia pekee ya kuhakikisha mwananchi wa kawaida anapata huduma.

image
na Davis Ojiambo

Habari13 June 2024 - 12:57

Muhtasari


  • •"Hawa waheshimiwa nataka tafadhali niwahakikishieni tafadhali pitisheni budget haraka hawa wakulima wanahitaji stima," alisema.  
RUTO

Rais William Ruto amewataka Wabunge kupitisha Bajeti ya 2024-25 ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.  

Akizungumza mjini Meru wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi kwa Kiwanda cha kusaga Mahindi cha Meru siku ya Alhamisi, Ruto alisema kwamba bajeti hiyo ndiyo njia pekee ya kuhakikisha mwananchi wa kawaida anapata huduma kama vile umeme. 

"Hawa waheshimiwa nataka tafadhali niwahakikishieni tafadhali pitisheni budget haraka hawa wakulima wanahitaji stima," alisema.  

Rais pia alisisitiza kuwa katika mwaka ujao wa fedha, lengo kuu litakuwa katika ujenzi wa barabara, kuunganisha umeme na maji.

 "Tayari tumeweka mpango wa bajeti yetu," alisema Pia aliangazia juhudi za serikali za kuhakikisha kuwa kila mfugaji wa maziwa anapata Sh50 kwa lita ya maziwa kuanzia Julai mwaka huu.  

Waziri wa fedha Njuguna Ndung’u alisoma bajeti ya Mwaka wa Fedha wa 2024-25 siku ya Alhamisi, katika majengo ya Bunge. 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved