Tume ya Kupambana na Maadili na Rushwa (EACC) imewakamata wafanyikazi 11 wa kaunti ya Vihiga kufuatia ufujaji wa takriban shilingi milioni 17 zilizotengwa kwa ujenzi wa kituo cha kuongeza damu katika kaunti hiyo.
Wakizungumza na Citizen mnamo Alhamisi, tume ya EACC ilisema kuwa iliwakamata Afisa Mkuu wa Huduma za Matibabu, Dkt. Arnold Kimiyia Mamadi, na Mkurugenzi wa Manunuzi, Godfrey Oyaro ambao walikuwa wanatarajiwa kufika korti ya Kakamega mnamo Alhamisi.
Mshukiwa wa 12 ni Eugene Wandera Wamalwa, ambaye inasemekana yuko mafichoni, na mahakama imempa amri ya kufika kwenye tume ya EACC katika afisi ya Kisumu.
Wakithibitisha kukamatwa kwao, msemaji wa EACC, Eric Ngumbi, alisema kuwa washukiwa hawa waliharibu mali ya umma ya takriban shilingi milioni 17.
Ufujaji wa hela hizi adhimu ulifanyika kupitia vizuka vilevile kupitia malipo ya kazi ambazo hazipo.
Kandarasi hii ililenga katika kufanya ujenzi wa kituo cha usambazaji damu kwa wagonjwa wanaohitaji huduma hii muhimu katika kaunti ya Vihiga.
Washukiwa hao, inasemekana walilala katika rumande ya bandari ya Kisumu na wanatarajiwa kufika kwenye korti ya Kakamega kujibu tuhuma zinazowakabili mnamo Alhamisi hii leo.
Hatua hii ya EACC inawasili baada ya uchunguzi wa muda mrefu kubainisha mahusiano ya ufujaji wa fedha za umma kwa njia isiyofaa.
Mbali na hayo,Tume ya kupambana na Maadili na Rushwa inatarajiwa katika usaidizi wa kupambana na wizi na ufisadi katika sekta ya afya nchini kwani ni wanyonge ndio wanaokandamizwa hasa wanapoenda kutafuta huduma za matibabu hospitalini.