logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanamume azirai na kuaga akitoa ushahidi kortini Bondo

Hamna rekodi ambazo zilipatikana kufuatia matibabu ya Obonyo kwenye hosptali hiyo.

image
na Davis Ojiambo

Habari14 June 2024 - 10:06

Muhtasari


  • •Marehemu alifariki akiwa kwenye harakati za kupokea matibabu na huduma ya kwanza.
  • •Familia iliuchukua mwili wa marehemu nyumbani mighairi ya kujaza ripoti yoyote kuhusu kifo cha Obonyo.

Familia ya mwanamume mmoja katika kaunti ya Bondo kaunti ya Siaya wanaomboleza kifo cha mwendani wao aliyeanguka na kupiga dunia teka wakati alipokuwa akiwasilisha ushahidi kuhusu kesi iliyohusiana na urithi wa ardhi katika mahakama kuu ya Bondo.

Inasemekana, Obonyo alianguka katika masaa ya mchana na kupelekwa kwenye zahanati moja ya kibinafsi na familia ambapo iliripotiwa kuwa marehemu alifariki akiwa kwenye harakati za kupokea matibabu na huduma ya kwanza.

Kamanda wa polisi wa kaunti hiyo ya Siaya, bwana Cleti Kimaiyo, aliripoti kuwa, kisa hicho kilikuwa kimewasilishwa hapo awali kwenye kituo cha polisi cha Bondo na bwana Dick Ochiel ambaye ndiye msimamizi wa mahakama ya sheria ya Bondo.

Hata baada ya kufuatilia kisa hicho katika hosptali ya gatuzi la Bondo, ilibainika kuwa, hamna rekodi ambazo zilipatikana kufuatia matibabu ya Obonyo kwenye hosptali hiyo.

Uchunguzi wa kina ulibainisha kuwa familia ya Obonyo ilikuwa imempeleka marehemu katika hospitali ya Bama ambayo tawi lake limo Bondo.

Baada ya kuthibitisha kifo chake Obonyo,inasemekana kuwa familia iliuchukua mwili wa marehemu nyumbani mighairi ya kujaza ripoti yoyote kuhusu kifo cha Obonyo.

Bwana Kimaiyo alithibitisha msururu huu wa matukio yayo hayo moja kwa moja na akabainisha kwa bayana kuwa familia haikuwasilisha ripoti yoyote rasmi kuhusu kifo cha marehemu Obonyo katika kituo cha polisi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved