logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Worldcoin kurejelea shughuli zao nchini Kenya baada ya uchunguzi dhidi yao kusitishwa

Asasi za usalam nchini Kenya ambazo zilikuwa zinachunguza shughuli zao nchini Kenya.

image
na Davis Ojiambo

Habari20 June 2024 - 11:59

Muhtasari


  • • "Tunashukuru kwa uchunguzi wa haki wa DCI na kwa uamuzi wa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma kumaliza suala hilo," Scott alinukuliwa katika ripoti hiyo ya Reuters.
Worldcoin

Shirika linaojihusisha na biashara za pesa za kidijitali, Worldcoin liko huru kurejelea shughuli zao nchini Kenya, karibia mwaka mmoja baada ya shughuli zao kusitishwa mwaka jana.

Kwa mujibu wa taarifa ya shirika la habari la Reuters, asasi za usalam nchini Kenya ambazo zilikuwa zinachunguza shughuli zao nchini Kenya.

Mamlaka zilisimamisha Worldcoin mnamo Agosti mwaka jana, kufuatia pingamizi la faragha kuhusu kuchanganua mboni za watumiaji ili kubadilishana na kitambulisho cha kidijitali ili kuunda "utambulisho na mtandao mpya wa kifedha".

Worldcoin inazinduliwa na Tools for Humanity, kampuni iliyoanzishwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa OpenAI Sam Altman. Tovuti yake inasema imesajili watumiaji milioni 5.7 katika zaidi ya nchi 160.

"Baada ya kukagua faili hiyo, Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma ... aliagiza kwamba faili hiyo ifungwe bila hatua zozote za polisi," Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ya Kenya (DCI) iliandika katika barua ya Juni 14 kwa Coulson Harney, kampuni ya mawakili inayowakilisha Worldcoin kwa mujibu wa ripoti ya Reuters.

Worldcoin itaanza tena usajili wa watumiaji kote nchini Kenya hivi karibuni, alisema Thomas Scott, afisa mkuu wa sheria katika Tools for Humanity, katika taarifa.

"Tunashukuru kwa uchunguzi wa haki wa DCI na kwa uamuzi wa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma kumaliza suala hilo," Scott alinukuliwa katika ripoti hiyo ya Reuters.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved