logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Bobi Wine aunga mkono maandamano ya kupinga mswada wa Fedha hapa Kenya

Akielezea kufurahishwa kwake na waandamanaji wanaopinga mswada wa fedha,

image
na Davis Ojiambo

Habari24 June 2024 - 07:27

Muhtasari


  • •Katika taarifa aliyochapishwa Jumapili, Juni 23, 2024, kupitia ukurasa wake rasmi wa mitandao ya kijamii, Bobi Wine aliwapongeza vijana wa Kenya kwa kujitokeza mitaani kutumia haki zao za kidemokrasia kutoa malalamiko yao.
Bobi Wine

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, mwanaharakati wa kisiasa na mwanamuziki wa Uganda Robert Kyagulanyi Ssentamu maarufu kama Bobi Wine amefichua kuwa anaunga mkono maandamano yanayoendelea nchini dhidi ya mswada Mswada wa Fedha.

Katika taarifa aliyochapishwa Jumapili, Juni 23, 2024, kupitia ukurasa wake rasmi wa mitandao ya kijamii, Bobi Wine aliwapongeza vijana wa Kenya kwa kujitokeza mitaani kutumia haki zao za kidemokrasia kutoa malalamiko yao.

Akielezea kufurahishwa kwake na waandamanaji wanaopinga mswada wa fedha, Bobi Wine alifichua kuwa sauti za waandamanaji zinasikika mbali Zaidi ya mipaka ya Kenya.

“Mnaongea na sauti zenu zinasikika mbali zaidi ya mipaka ya Kenya. Tunaendelea kusimama pamoja wakati mnapopingania haki zenyu.” Alisema.

Kiongozi huyo wa upinzani nchini Uganda, alisema kuwa ana matumaini sauti za waandamanaji zitasikizwa na serikali ya Kenya na kuongeza kuwa ataendelea kusimama kidete na waandamanaji wanaopinga mswada wa Fedha.

“Tunatumai viongozi  pia wanasikiliza! Tunaendelea kusimama kwa mshikamano nanyi, nguvu kwenu vijana wa Kenya.” Alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved