logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mtu mmoja afariki na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mkutano wa kampeni za uchaguzi Rwanda

Paul Kagame na chama chake cha RPF Inkotanyi hawajatoa maoni yao kuhusu kifo hicho.

image

Habari24 June 2024 - 12:32

Muhtasari


  • Kampeni za uchaguzi mkuu wa Julai mosi zilianza Jumamosi, huku Bw Kagame akifanya mikutano miwili kaskazini mwa Rwanda mwishoni mwa juma.

Mtu mmoja amefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati wa mvutano kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi wa rais wa Rwanda Paul Kagame, maafisa wanasema.

Kampeni za uchaguzi mkuu wa Julai mosi zilianza Jumamosi, huku Bw Kagame akifanya mikutano miwili kaskazini mwa Rwanda mwishoni mwa juma.

Ajali hiyo ilitokea Jumapili wilayani Rubavu, ambapo watu 37 walijeruhiwa, wanne kati yao wamelazwa hospitalini wakiwa na majeraha mabaya, taarifa ya wizara ya serikali za mitaa ilisema.

Iliomba msamaha kwa familia ya marehemu, na kuongeza kuwa timu ya matibabu kwenyeeneo la mkasa "ilifanya kila linalowezekana".

Bw Kagame anawania muhula wa nne. Amekuwa kiongozi mkuu wa nchi hiyo tangu 1994, wakati kundi lake la waasi la wakati huo, Rwanda Patriotic Front, lilipotwaa mamlaka mwishoni mwa mauaji ya kimbari yaliyoelekezwa kwa watu wa kabila lake la Watutsi.

Alishinda uchaguzi uliopita wa urais mnamo 2017 kwa karibu 99% ya kura.

Rais huyo mwenye umri wa miaka 66 amekabiliwa na ukosoaji kutoka kwa makundi ya kutetea haki za binadamu kwa kukandamiza upinzani - lakini ametetea vikali rekodi ya Rwanda kuhusu haki za binadamu, akisema nchi yake inaheshimu uhuru wa kisiasa.

Baada ya mkanyagano wa Jumapili, wizara ya serikali za mitaa iliwakumbusha "wale wanaoshiriki katika shughuli za kampeni... kufuata maagizo yaliyotolewa na wasimamizi ili kuhakikisha usalama na utulivu wa wale wanaoshiriki katika shughuli za kampeni".

Paul Kagame na chama chake cha RPF Inkotanyi hawajatoa maoni yao kuhusu kifo hicho.

Hata hivyo, Jumatatu asubuhi, RPF Inotanyi ilichapisha video kwenye Facebook ya Bw Kagame akipanda jukwaani kwenye mkutano huo. Takriban watu 250,000 walihudhuria mkutano huo.

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved