logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Maduka yafungwa, usafiri kulemazwa huku maandamano Kisumu yakianza

Maduka yamefungwa huku maandamano yakianza katika jiji la kisumu.

image
na Davis Ojiambo

Habari25 June 2024 - 09:54

Muhtasari


  • •Biashara katika mji  huo zilibaki zikiwa zimepooza, huku maduka yakiwemo maduka makubwa yaliyokuwa yamefunguliwa mapema yakifungwa saa 9 asubuhi.
  • •Usafiri pia uliathirika pakubwa, huku magari machache yakionekana kukwama barabarani.
kundi la vijana wakiandamana kule kisumu,Jumanne Juni 25 2024

Waandamanaji wa kupinga mswada wa fedha mjini Kisumu walimiminika katika mitaa mbalimbali ya Jiji kuunga mkono mwito wa 'Kataa Mswada wa Fedha'.

Waandamanaji waliokuwa na amani walivamia barabara za jiji la kando ya ziwa wakiwa na mabango, nyimbo, densi na kuimba nyimbo za kumpinga Rais William Ruto.

Vijana hao walikuwa wamekusanyika katika viwanja vya Kondele mapema saa tisa alfajiri ambapo walianza kusonga mbele kwa makundi na hatimaye kuanza maandamano.

“Hatutachoka kuandamana, huu ni wakati wetu na tutawafundisha somo,” alifoka kijana mmoja.

Biashara katika mji huo zilibaki zikiwa zimepooza, huku maduka yakiwemo maduka makubwa yaliyokuwa yamefunguliwa mapema yakifungwa saa 9 asubuhi.

Usafiri pia uliathirika pakubwa, huku magari machache yakionekana kukwama barabarani. Maafisa wa polisi waliwafuatilia waandamanaji barabarani.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved