logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wabunge wapitisha marekebisho ya muswada wa fedha 2024,wasubiri kura ya mwisho

Inatarajiwa kuidhinishwa kwa Mswada huo kutafanywa wakati wowote katika wiki.

image

Habari25 June 2024 - 11:42

Muhtasari


  • Mswada huo ulipitishwa baada ya kuungwa mkono na wabunge wengi wa Kenya Kwanza. Wabunge wa Azimio walikataa Mswada huo kabisa.
Bunge la Kenya

Wabunge mnamo Jumanne, Juni 25 walipitisha Mswada wa Fedha wa 2024 pamoja na marekebisho yake.

Mswada huo ulipitishwa baada ya kuungwa mkono na wabunge wengi wa Kenya Kwanza. Wabunge wa Azimio walikataa Mswada huo kabisa.

Wabunge 195 walipiga kura kupitisha Mswada huo pamoja na marekebisho huku Wabunge 106 wakipiga kura ya NO.

Mswada huo sasa utaendelea kusomwa kwa Mara ya Tatu kabla ya kupelekwa kwa Rais William Ruto ili kupata kibali.

Inatarajiwa kuidhinishwa kwa Mswada huo kutafanywa wakati wowote katika wiki.

Mswada huo ulipitishwa baada ya Wabunge kupiga kura ili mswada huo uendelee kusomwa kwa Mara ya Tatu baada ya kupiga kura kuhusu marekebisho yaliyopendekezwa.

Mswada huo umepitishwa chini ya saa mbili, kufuatia wabunge wa upinzani kuondoa mapendekezo yao wakisema kwamba hawataki kushiriki kwa vyovyote katika uundaji wa sheria hiyo.

Hii inamaanisha kwamba mswada huo ambao umeibua pingamizi kote nchini kutokana na vipengele vya ushuru mpya, unapigiwa kura ya mwisho na ukipita kama inavyotarajiwa, utapelekwa Ikulu ya Nairobi kutiwa sahihi na Rais William Ruto na kuwa sheria wakati wowote wiki hii.

Haya yanajiri huku kukiwa na maandamano makubwa katika miji mbali mbali nchini na kampeni mitandaoni zilizotaka mswada huo ukataliwe wote ulivyo.

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved