logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kwa nini vijana wa Gen-Z waandamana?

vijana walibeba vibango vilivyopitisha ujumbe wa kushutumu utekaji wa kimabavu wa vijana.

image
na Davis Ojiambo

Habari26 June 2024 - 07:24

Muhtasari


  • •“Tumehuzunika sana Ruto kuangusha nyumba za mababu zetu! Kuja kuchukua jasho za mababu zetu na kunyanyasa vijana. Anataka sisi vijana tuende wapi? Tugeuke tuwe majambazi na kutumia visu kuibia watu? Wakenya fanyaje?” Alisema Waingo akizungumza nasi.
  • •Vijana walibeba vibango vilivyokuwa vikipitisha ujumbe wa kushutumu utekaji wa kimabavu wa vijana waliokuwa wanatumia uhuru wao wa maoni
  • •Vijana hawana kazi, rasilimali za nchi zamezwa na ufisadi, polisi wanatuua kiholela, mamamboga hana riziki, ushuru umekuwa ghali na wananchi wanaaumia. Haki iwe ngao na mlinzi,” alimalizia mwandamanaji mmoja 

Taifa la Kenya limekuwa likishuhudia hali ya mshikemshike kufuatia maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha wa 2024 huku vijana wakitoa sababu kuu za kwa nini wanaandamana.

Vurugu na patashika zilikithiri katika maandamano hayo ya jana huku wafanyibiashara wakipoteza  maelfu ya mali yao.

Aidha mali ya umma hayakusazwa kwani wananchi walijishirikisha katika uharibifu wa mali ya umma kama barabara na hata uteketezaji wa nyumba na magari ya serikali.

“Sisi hatutambui Ruto tunatambua Kibaki. HE’S THE REAL ECONOMIST!” Alisema mwandamanaji mmoja.

Uongozi wa rais William Ruto umezidi kupata kejeli na upinzani mkali kutoka kwa vijana machachari wa kizazi cha Gen Z huku wengi wakiapa kuwa mswada wa fedha wa mwaka 2024 hautatiwa sahihi kama inavyotarajiwa wiki ijayo.

“Kama wakoloni walirudi ng’ambo Sugo shi’ngapi?’’ kibango kimoja kilisoma.

“Tumehuzunika sana Ruto kuangusha nyumba za mababu zetu! Kuja kuchukua jasho za mababu zetu na kunyanyasa vijana. Anataka sisi vijana tuende wapi? Tugeuke tuwe majambazi na kutumia visu kuibia watu? Wakenya fanyaje?” Alisema Waingo akizungumza nasi.

Fauka ya hayo, vijana walisikitika kwa kuwa serikali inayofaa kuwa ya huru na haki ndiyo inayodhihaki haki zao.

“Nimehuzunika sana kuwa kwenye jiji la Nairobi. Kuna kijana Fulani ameuwawa kwa kupigwa risasi ya tumbo na kichwa. Mambo yenye Ruto anafanya huku mjini nimehuzunika sana!” Aliendelea Waingo aliyetamaushwa na mauji hayo ya kinyama.

Kando na hayo, vijana walibeba vibango vilivyokuwa vikipitisha ujumbe wa kushutumu utekaji wa kimabavu wa vijana waliokuwa wanatumia uhuru wao wa maoni.

Wananchi walibeba bendera ya Kenya huku wakiimba wimbo wa taifa kuonyesha uzalendo na upendo wa juu wan chi.

“Tunatoa ushuru ila hamna maendeleo tunayoyashuhudia. Vijana hawana kazi, rasilimali za nchi zamezwa na ufisadi, polisi wanatuua kiholela, mamamboga hana riziki, ushuru umekuwa ghali na wananchi wanaaumia. Haki iwe ngao na mlinzi,” alimalizia mwandamanaji mmoja huku akinukuu wimbo wa taifa.

Iwapo viongozi hawatajipiga msasa na kusimama kidete basi huenda hali ikawa mbaya zaidi huku vijana wakisubiri Alhamisi warudi tena katika kuandamana mpaka haki zao zisikilizwe.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved