logo

NOW ON AIR

Listen in Live

JSC yasitisha Uajiri wa Majaji wa Rufaa kutokana na kupunguzwa kwa bajeti

Idara ya Mahakama ilitazamiwa kupokea Ksh.24 bilioni kufadhili gharama zote lakini kwa agizo hilo jipya, zitatengewa Ksh.20 bilioni.

image
na Davis Ojiambo

Habari03 July 2024 - 13:41

Muhtasari


  • •Katika bajeti ya 2024/25, Idara ya Mahakama ilitazamiwa kupokea Ksh.24 bilioni kufadhili gharama zote lakini kwa agizo hilo jipya, zitatengewa Ksh.20 bilioni.
  • •Rais Ruto  alibainisha kuwa gharama za bajeti kwa afisi za Mke wa Rais na na wa naibu wa Rais zitafutiliwa mbali.

Tume ya Huduma za Mahakama (JSC) imesitisha uajiri wa majaji wa Mahakama ya Rufaa kufuatia kupunguzwa kwa asilimia 15 ya bajeti ya ugawaji wa bajeti ya Hazina ya Kitaifa.

Katika bajeti ya 2024/25, Idara ya Mahakama ilitazamiwa kupokea Ksh.24 bilioni kufadhili gharama zote lakini kwa agizo hilo jipya, zitatengewa Ksh.20 bilioni.

Kulingana na mwenyekiti wa JSC Jaji Mkuu Martha Koome, agizo hilo litakuwa na madhara makubwa katika utendakazi wa Mahakama.

Hivyo kuhitaji marekebisho makubwa ya mipango iliyopangwa ikiwa ni pamoja na kusimamisha uajiri wa majaji 11 wa Mahakama ya Rufaa ambao ulipangwa kuanza Jumatano.

Koome alisema kuwa kesi zinazosubiri kutekelezwa zitaathirika.

“Hivi sasa, Mahakama ya Rufaa ina jumla ya Majaji 29 wanaohudumu katika vituo sita pekee nchi nzima ikiwa na maana ya benchi 9 kwa wakati wowote

Mahakama hiyo ilikuwa na jumla ya kesi 13, 331 hadi kufikia Mei 2024 ambazo asijatatuliwa,” ilisema taarifa hiyo. 

Zaidi ya hayo, JSC ilidokeza kuwa kifo cha Hakimu Monica Kivuti wa Mahakama ya Sheria ya Makadara kililazimu kufanyiwa marekebisho na kugawanywa upya kwa bajeti ili kutimiza mipango ya usalama ili kutoa mazingira salama kwa watumiaji wote wa mahakama.

"Kwa hivyo Mahakama itahitaji rasilimali za ziada katika Mwaka wa Fedha wa 2024/2025 kushughulikia maswala haya ya haraka."

CJ Koome aliahidi kushirikisha Bunge na watendaji ili kuimarisha na kupata bajeti ya Mahakama.

Maagizo hayo mapya yanaambatana na hatua za kubana matumizi yalizoahidiwa na Rais William Ruto za kukata pande zote za serikali kufuatia kukataliwa kwa Mswada wa Fedha.

Ruto pia alibainisha kuwa gharama za bajeti kwa afisi za Mke wa Rais na na wa naibu wa Rais zitafutiliwa mbali.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved