logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Tazama maeneo ambako stima zitapotea leo, Jumatano- KPLC

Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Kisumu, Nyeri, Tharaka Nithi.

image
na SAMUEL MAINA

Habari03 July 2024 - 04:20

Muhtasari


  • •KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Julai 3. 
  • •Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Kisumu, Nyeri, Tharaka Nithi.

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Julai 3. 

Katika taarifa ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti nne za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Kisumu, Nyeri, Tharaka Nithi.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu kadhaa za mtaa wa Eastleigh zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za eneo la Chiga katika kaunti ya Kisumu zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.

Sehemu kadhaa za soko ya Gikumbo na soko ya Gaikuyu zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Tharaka Nithi, sehemu kadhaa za maeneo ya Chuka na Kimbumbu yatokosa umeme kati ya saa mbili unusu na saa kumi na moja jioni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved