logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Bondi ya jamaa aliyeshtakiwa kwa kuiba nyama 181kgs yapunguzwa kutoka Sh10m hadi Sh150k

Mawakili wa Azimio wakiongozwa na mwanasiasa Babu Owino waliingilia kati na kumtuma wakili wao.

image
na Davis Ojiambo

Habari04 July 2024 - 07:44

Muhtasari


  • • Paul Mutua alifikishwa katika mahakama mjini humo na kushtakiwa kwa visa vya uhalifu wa mali na wizi wakati wa maandamano ya wiki jana ya kupinga mswada wa fedha wa mwaka 2024.
  • • Jumanne, mahakama ilimuachilia kwa dhamana ya shilingi milioni 10, jambo ambalo lilizua vilio na malalamiko mengi kutoka kwa umma.
Mahakama

Baada ya kilio kingi kutoka kwa umma kuhusu dhamana aliyoachiliwa jamaa mmoja anayeshukiwa kwa wizi wa nyama na vitu vingine mjini Eldoret, mahakama kuu sasa imeingilia kati na kupunguza dhamana hiyo.

Paul Mutua alifikishwa katika mahakama mjini humo na kushtakiwa kwa visa vya uhalifu wa mali na wizi wakati wa maandamano ya wiki jana ya kupinga mswada wa fedha wa mwaka 2024.

Jumanne, mahakama ilimuachilia kwa dhamana ya shilingi milioni 10, jambo ambalo lilizua vilio na malalamiko mengi kutoka kwa umma.

Mawakili wa Azimio wakiongozwa na mwanasiasa Babu Owino waliingilia kati na kuandikia mahakama kuu ya Eldoret barua wakitaka dhamana ya Mutua kuangaziwa upya.

"Kupitia kwa Wakili wetu Aseso Omollo tulitafuta Mapitio ya masharti ya bondi kutoka kwa shilingi milioni 10 ambayo aliwekewa Jonathan Mutua kwa madai ya kuiba kilo 181 za Nyama huko Eldoret hadi dhamana ya pesa taslimu ya shilingi 150K," alifichua MP Babu Owino.

Mahakama, ilipokagua Jumatano, ilimwachilia mshukiwa kwa dhamana ya pesa taslimu Ksh.200,000, kwa chaguo la bondi ya Ksh.150,000

Alishtakiwa kwa kuingia katika Ukumbi wa Baniyas Club Square unaomilikiwa na kuiba vitu vya thamani ya Ksh.37,093,690.

Vitu vilivyoibiwa ni pamoja na skrini za televisheni, kompyuta, printa, mitungi ya gesi, viti, kochi la mgahawa, vyombo, vyakula, mkaa, kilo 181 za nyama ya ng’ombe, magunia 17 ya mkaa na magunia 12 ya viazi.

Mutua, 29, hata hivyo alikanusha mashtaka hayo alipofika mbele ya Hakimu Mkuu wa Eldoret Cherono Kesse. Kesi hiyo imepangwa kutajwa Julai 15, 2024.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved