logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mahakama yawaachilia waandamanaji 187 kwa dhamana

Takriban waandamanaji 187 wameachiliwa kwa dhamana baada ya kukamatwa Jumanne

image
na Davis Ojiambo

Habari04 July 2024 - 08:28

Muhtasari


  • •Mahakama ya Milimani imeamuru takriban  waandamanaji 187 waliokamatwa kuachiliwa kwa dhamana.
  • •Jumla ya watoto 18 kuachiliwa kwa dhamana ya ksh.10,000 itakayoshikiliwa na wazazi wao na walezi wao ilhali watu wazima Ksh.50,000
Mahakama ya Milimani mjini Nairobi

Mahakama imeamuru waandamanaji waliokamatwa kuachiliwa kwa dhamana baada ya kushikwa wakati wa maandamano ya kupinga mswada wa fedha 2024.

Kwenye kikao cha mahakama ya Milimani Julai 3,usiku ili kusikiliza kesi ambapo watu 187 waliojumuisha watoto 18 walishtakiwa kufuatia maandamano ya Jumanne jijini Nairobi.

Hakimu mkuu mwandamizi Wandia Nyamu aliagiza kwamba watoto hao 18 waachiliwe huru mara moja kwa dhamana ya kibinafsi ya Ksh 10,000 itakayoshikiliwa na wazazi na walezi wao.

Hakimu huyo aidha, alisema kuwa haki za watoto hao zimekiukwa kwa kuwa wamewekwa kwenye seli moja na watu wazima, wengine wamejeruhiwa na hawajahudumiwa na hawajalishwa kwa muda wote waliokaa.

Hata hivyo,hakimu mkuu aliagiza kwamba watu wazima waachiliwe ifikapo saa 10 asubuhi kwa bondi za kibinafsi za Ksh 50,000 leo Julai 4. Alisema hilo linapaswa kufanywa baada ya maelezo ya kibinafsi ya walalamikiwa kuchukuliwa na maafisa wa uchunguzi.

Waandamanaji hao walifikishwa kwenye mahakama ya Milimani Julai 2 baada ya kukamatwa. Wakati wa kukamatwa kwao walikuwa wakipaza sauti  wakisema; 'Hatuna hatia'

Maandamano yamekuwa yakienea nchini kwa takriban wiki tatu sasa,huku viongozi mbalimbali kama vile naibu rais Rigathi Gachagua wakitaka vijana kukomesha maandamano.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved