logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Millicent Omanga amjibu jamaa aliyemrushia mistari

Millicent Omanga amemjibu jamaa aliyemrushia mistari ya kumtongoza

image
na Davis Ojiambo

Habari04 July 2024 - 09:24

Muhtasari


  • •Jamaa aliandika ujumbe kwenye kundi moja la Facebook akidai kuwa Millicent Omanga hummaliza kutokana na urembo wake huku akiomba nafasi ya mapenzi.
  • •Omanga kwa upande wake alionyesha kufurahia huku akiandika 'Ni kama nimefikiwa' kwenye ukurasa wake wa X almaarufu twitter.
Millicent Omanga

Mwanasiasa ,Millicent Omanga ameguswa na ujumbe wa mapenzi kutoka kwa mwanamume ambaye aliamua kufunguka roho yake.

Jamaa mmoja alichapisha kwenye Facebook akidai kuwa MIllicent Omanga ni miongoni mwa wanawake waliobarikiwa kwa urembo.

"Nimekuwa nikifikiria juu yako siku nzima na jinsi unavyomaanisha kwangu. Wewe ni mwanamke mrembo zaidi ambaye nimewahi kuona-mrembo, mcheshi, mwerevu na mkarimu. Mwanamume yeyote angebahatika kuwa nawe. Nitakapokuwa na wewe, tuonane, moyo wangu unaruka ruka kidogo, na ninatumaini utanipa nafasi wakati wowote utakaponihitaji nitakufanyia chochote , heshima, na kukuunga mkono," aliandika.

Hata hivyo, alimsihi Omanga kujibu ujumbe wake hata kama mapendekezo yake yangekataliwa.

"Nilifikiri kushiriki hisia hizi itakuwa vigumu, lakini kwa uaminifu, kukuambia jinsi ulivyo wa ajabu ni rahisi sana. Wazo la wewe kusoma barua hii na kujisikia kupendwa, kuthaminiwa, na kuthaminiwa huniletea furaha kubwa. Umegusa maisha yangu katika hali kama hiyo. njia nzuri ambayo siogopi tena kwa kuwa wewe. Haijalishi unajisikiaje, tafadhali niandikie hata kama haifanyi kazi kimapenzi, ningethamini jibu lako milele."

Omanga alionyesha kufurahishwa huku akieka chapisho kwa ukurasa wake wa  X almaarufu twitter.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved