logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mshukiwa akamatwa na bangi ya thamani ya Sh600,000

Mwanaume mmoja amekamatwa baada ya kupatikana na bangi ya thamani ksh.600,000

image
na Davis Ojiambo

Habari04 July 2024 - 09:01

Muhtasari


  • •Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) katika taarifa Alhamisi ilisema mshukiwa alikamatwa kando ya barabara ya  Eastern Bypass.
    •Kukamatwa kwa mtu huyo kunafuatia taarifa za kijasusi, ambazo zilisababisha kukamatwa kwa gari alilokuwa akiendesha.

Polisi jijini Nairobi wanamshikilia mwanamume mmoja kwa tuhuma za ulanguzi wa mihadarati.

Idara ya upelelezi wa jinai (DCI) katika taarifa Alhamisi ilisema mshukiwa alikamatwa kwenye barabara ya  Eastern Bypass. DCI ilisema bangi ambayo thamani yake ya mtaani inakadiriwa kuwa Sh600,000 ilipatikana wakati wa operesheni hiyo.

Kulingana na DCI, kukamatwa huko kunafuatia maafisa wa kijasusi, ambao walisababisha kukamatwa kwa gari alilokuwa akiendesha mwanamume huyo na kikosi cha kupambana na mihadarati.

"Mmea ambao ulikuwa umefichwa kwenye mfuko wa gunia ndani ya  marobota manne na gari umezuiliwa kama vielelezo vinavyosubiri kufikishwa mahakamani kwa mshukiwa," DCI ilisema.

Mshukiwa huyo kwa sasa anazuiliwa katika kituo cha polisi jijini Nairobi. Haya yanajiri takriban wiki tatu baada ya maafisa wa polisi kutoka kitengo cha kupambana na mihadarati kunasa magunia saba ya bangi mjini Kilifi.

Bangi hiyo ilikuwa na uzito wa kilo 429.3 na ilikuwa na thamani ya mtaani ya Sh12,879,000.Afisa wa uchunguzi wa jinai katika kaunti ya Kilifi David Sielle alisema bangi hiyo ilinaswa katika eneo la Kibao Kiche kando ya barabara kuu ya Mariakani Mavueni. CCIO ilisema bangi hiyo ilipakiwa kwenye lori  na washukiwa wawili kukamatwa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved