logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Charlene awataka wakenya kumshirikisha Ruto kwenye X Space

Charlene alitoa changamoto kwa vijana kukumbatia ishara ya Ruto ya kukutana nao katika harakati za kutatua tatizo zao.

image
na Davis Ojiambo

Habari05 July 2024 - 07:05

Muhtasari


  • •Charlene alitoa changamoto kwa vijana kukumbatia ishara ya Ruto ya kukutana nao katika harakati za kutatua tatizo zao.
  • •Rais William Ruto anatazamiwa  kuwa mwenyeji wa mazungumzo yake ya kwanza ya X-Space (zamani Twitter) na vijana wa Kenya mwendo wa saa nane mchana hadi saa kumi na moja jioni leo.
Charlene Ruto

Binti wa kwanza Charlene Ruto amewataka vijana kujiunga na mkutano wa mtandao wa X Space na Rais William Ruto ili kueleza wasiwasi wao kufuatia maandamano ya hivi majuzi yaliyokumba maeneo kadhaa nchini.

Katika taarifa yake kupitia mtandao wa X , Charlene alitoa changamoto kwa vijana kukumbatia ishara ya Ruto ya kukutana nao katika harakati za kutatua changamoto za maandamano.

"Vijana, nafasi ya maisha inawangojea. Ninawahimiza kuitumia kwa busara na kushiriki kwa njia yenye kujenga kwa sababu nyinyi ndio mtakaoamua mwendelezo wa viwango hivyo vya mijadala kwa mafanikio yenu,” Charlene alisema.

Rais William Ruto anatazamiwa  kuwa mwenyeji wa mazungumzo yake ya kwanza ya X-Space (zamani Twitter) na vijana wa Kenya mwendo wa saa nane mchana hadi saa kumi na moja jioni leo.

Kulingana na Ikulu, baraza la mawaziri limepangwa kujiunga na majadiliano ya mtandaoni ya saa tatu. 'X Spaces', ni kipengele kinachokuruhusu kuwa na mazungumzo ya moja kwa moja ya sauti kwenye jukwaa la mitandao ya kijamii.

Tangazo hilo lilitolewa katika vyombo vya habari baada ya kikao cha baraza la mawaziri kilichoongozwa na rais kwenye  Ikulu ,Alhamisi Julai 5 ,2024.

Wakenya wamealikwa kujiunga na mjadala wa X Space kuanzia saa nane mchana hadi saa kumi na moja jioni.

"Wakenya wote wanakaribishwa kuchangia mazungumzo haya kama sehemu ya juhudi zetu za pamoja za kukuza upya wa kitaifa na kuunda Kenya bora kwa wote," 

Maendeleo hayo yanakuja kufuatia maandamano ya Gen Zs kushinikiza mageuzi ya utawala. Maandamano ya awali ya kitaifa dhidi ya mswada wa fedha wa 2024 ambao umetupiliwa mbali, yalishuhudia maelfu ya vijana wa Kenya wakiingia mitaani kwa wiki mbili.

Katika mahojiano ya pamoja ya wanahabari kwenye televisheni hapo awali, mkuu wa nchi alisema yuko tayari kuwashirikisha vijana kwenye jukwaa analopenda.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved